Karibu Musoma Information Center kwa huduma zifuatazo:- 1) Kwa kutengenezewa design mbalimbali kama za Business card, Vipeperushi, mabango mbalimbali, kadi za Harusi za kisasa zaidi, kadi za mialiko mbalimbali, Vitambulisho vya wanafunzi wa sekondari na katika kampuni mbalimbali ( ID cards) na kadi nyinginezo zenye design ya kuvutia. 2) Kutengenezewa mabango ( Posters) mbalimbali zinazohusu biashara ya mhusika au bidhaa mbalimbali. 3) Kutengenezewa nembo ( LOGO) za kuhusiana kampuni au biashara yako. 4) Tunatengeneza tovuti ( Websites ) zenye kiwango ambacho huwezi amini kama zinatengenezwa musoma, kwa bei nafuu ambayo huwezi ipata kwingine isipo kuwa kwetu. 5) Mwisho tunatoa ushauri na elimu kuhusiana na maswala ya computer.5) Sisi ni watengenezaji wa blog zinazokaa mfumo wa website. kama hii unayoiona.

Welcome to TYPS - ASSOCIATION

Welcome to TYPS - ASSOCIATION

Welcome

A Letter from the Executive Director

Dear All,

As Executive Director it is my pressure to welcome you to TANZANIA YOUTH POTENTIALS ASSOCIATION (TYPs-ASSOCIATION)-a growing youth-led Organization with it’s headquarter in Musoma that operates through legal registration number 00NGO/00006304 under the ACT of 2002 in Tanzania. The focus of the organization is to utilize youth’s potentials for their own development, community and state development at large. It also intends to strengthen regional and international interventions towards protection and promotion of the human rights especially to children, youth and women. It works with networking with other partners/ stakeholders and beneficiaries.

The Organization has the mission of striving and inheriting youth and other community groups with various technical capacities eligible to make them be engines for socio-economic growth for individual benefits, societies and the national at large as such to see a community in which women’s and children’s rights are observed and respected by executing mobilization projects eligible to bring positive changes to community through action and participation in collaboration with community and other stakeholders to prevent Gender Based Violence (GBV).

However the organization is dedicated to develop dynamic and entrepreneurial youths who will engage and realize their full potential and that of their community, their country and the world at large and advocating The National Youth Development Policy

The Secretariat , the Board of Directors and the Annual General Meeting of TYPs-ASSOCIATION eagerly anticipate your arrival and contribution to its future, and welcome you to discover youth development experience that promotes your Personal and intellectual growth

Welcome to TYPs-ASSOCIATION,
Mr. Japheth M. Kurwa
Executive Director


MAENDELEO YA VIJANA: TUNAO WAJIBU WA KUFANYA

Thursday, October 16, 2014

Utangulizi
—  Changamoto ya maendeleo ya vijana ni suala mtambuka. Uwezeshaji wa vijana unajumuisha juhudi za pamoja za wadau mbalimbali muhimu pamoja na serikali, jamii, sekta binafsi, asasi za kijamii, familia na vijana wenyewe.
—  Kwa mujibu wa sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007; vijana fasili yake ni Vijana wa kiume na kike kuanzia umri wa miaka 15 hadi 35.
Wadau wa Maendeleo ya Vijana
Wadau wa maendeleo ya vijana ni pamoja na:-
  • Serikali
  • Jamii
  • Sekta binafsi
  • Asasi za kijamii
  • Familia
  • Vijana wenyewe
Kada, Ofisi, Idara na Taasisi za Umma Zinazoshughulika moja kwa moja na Masuala/ Maendeleo ya Vijana
—  Kada/ofisi ya Maendeleo ya Vijana; inaratibu masuala yote ya vijana
—  Kada/ofisi ya Utamaduni
—  Kada/ofisi ya Michezo
—  Kada/ofisi ya Maendeleo ya Jamii; kwa usajiri wa Vikundi
—  Kada/ofisi ya Ushirika; ushauri wa kitaalam na kisheria kuhusu ushirika wa vikundi kama vile SACCOS, VICOBA n.k na Usajili
—  Idara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana
—  VETA
Fursa za Vijana toka Serikalini
—  Mfuko wa Taifa wa Maendeleo ya Vijana; unatoa mikopo kwa vikundi vya maendeleo ya vijana nchini kote kupitia SACCOS za Vijana zinazoendelea kuudwa na vijana wenyewe kila halmashauri nchini
—  Mradi wa kufyatua Tofari wa Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) kwa halimashauri zote nchini
—  Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF); unatoa mikopo ya mitaji kwenye SACCOS zikiwemo zile za Vijana
—  Halmashauri; zina mfuko wa kukopesha/ kuwawezesha vikundi vya wanawake na vijana kupitia ofisi ya mtendaji wa kata na Kamati za Maendeleo ya Kata(WDC) n.k
Wosia kwa Vijana na Wadau wa Wamaendeleo ya Vijana
—  Taifa halimuangalii kijana kama tatizo bali kama rasilimali na nguvukazi ya kujenga uchumi wa Taifa
—  Taifa linatambua ushindani mkubwa wa kimaendeleo baina ya vijana na ubunifu walionao
—  Kuna kila haja ya kuwekeza zaidi katika ubunifu wa vijana (Youth initiatives) ili waweze kujiajiri na kuajiri vijana wenzao.
—  Tunao wajibu wakufanya; ikiwa ni pamoja na kuchangamkia fursa zote za maendeleo na kuzitumia vizuri.
—  Kwa changamoto ya mitaji inayotukabili vijana; tukumbuke umoja ni nguvu  hivyo yatupasa kuunda/ kuanzisha ushirika ili kuweza kupata mitaji
—  Vijana wengi hawana mahusiano mazuri na sekta rasmi, hivyo kila mdau atambue anao wajibu wa kufanya ili kusaidia suala la maendeleo ya vijana; hususani kijana mwenyewe

TUNAWEZA: MIRADI YA KILIMO

Monday, July 28, 2014





Kikundi cha TUNAWEZA ni ushirika wa hiari wa ujasiriamali wa kilimo, ufugaji na biashara kwa maendeleo ya wanakikundi, kikundi, jamii na taifa kwa ujumla. Kikundi hiki kipo Mtaa wa Kiara, Kata ya Kigera, Manispaa ya Musoma.

Katibu wa kikundi, Japheth M. Kurwa alisema yafuatayo “Tunaimani juu ya kilimo, na kwa sasa tunayo miradi miwili ya kilimo; wa kwanza ni mradi wa kilimo cha Mhogo katika eneo la Kisiwani-Kiara lililoko wilayani Manispaa ya Musoma, na kwa mradi huu tunazo ekari 5, na mradi wa pili ni kilimo cha zao la biashara la mahindi, katika eneo la bonde la mto Suguti lililoko wilayani Bunda mkoani Mara. Tunazo hekari 15 za mahindi tutakazolima msimu.

Miradi yote hii tunajikita katika kuzalisha katika hali ya ubora na ufanisi ili kupunguza balaa la njaa katika jamii na kwa taifa kwa ujumla, ikiwa ni pamoja na wanakikindi kujiajiri katika kilimo.

Pamoja na jitihada zote hizi katika kilimo bado tunakabiliwa na changamoto ya ukosefu mitaji ili tuweze kuwekeza na kuzalisha kwa ufanisi mkubwa. Tunaupungufu wa pembejeo za kilimo na nyenzo za kisasa ambayo huadhili miradi hii kwa kiasi kikubwa.

Changamoto ya pili ni ya mabadiliko ya tabia nchi, hii inatulazimu kununua machine za umwagiliaji kwani mvua sasa ni tatizo.
Kama kikundi tunayo mikakati madhubuti ya kuweza kupata mikopo na kwa sasa tumekwisha omba toka Halmashauri ya Manispaa ya Musoma kupitia fedha za vijana-Katani kufadhili mradi wa kilimo cha Muhogo, pia temeomba fedha toka Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo kupitia mfuko wa maendeleo ya vijana. Lakini pia wanakikundi tunao utaratibu wa kuchangia miradi hii. Mwenyezi Mungu akitujaharia kupata fedha hizi tunaamini kupitia kilimo tutafanya mambo makubwa.

Si sahihi kuwa na dhana kwamba kilimo cha biashara kinaweza kufanywa na watu wenye kipato cha kati na cha juu. Tumeanza mwaka jana miradi yote hii na sasa tumeona kuwa inawezekana na TUNAWEZA kwani wazo tunalo, watu tunao na kwa umoja wetu tutaujenga uchumi wetu”.

VIJANA MANISPAA YA MUSOMA KUAZIMIA KUUNDA CHAMA CHA AKIBA NA MIKOPO

Monday, April 14, 2014





CHAMA CHA USHIRIKA CHA AKIBA NA MIKOPO CHA VIJANA MUSOMA SACCOS (VIMU SACCOS) LTD
S.L.P …., Musoma-Mara. Simu: 0756290672, 0755671818, & 0654655498

Vijana wapatao 45, manispaa ya Musoma wameazimia kuunda na kusajiri Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo kijulikanacho kwa jina la VIJANA MUSOMA SACCOS LTD kwa lengo la kuinuana khali zao kiuchumi na kijamii.
Mwenyekiti wa Bodi ya uanzilishi wa Chama hicho, Bwn. Japheth M. Kurwa; alisema “Wanachama wa chama cha ushirika cha VIJANA MUSOMA SACCOS (VIMU SACCOS) tumeamua rasmi na kwa dhati kusaidiana, kushirikiana, kuthaminiana, kujaliana, kujiendeleza na kusimamia ubora wa maisha yetu ili kila mmoja apate unafuu na furaha katika maisha kwa kuzingatia misingi ya uhuru, haki, udugu na amani, Madhumuni ya chama hiki cha ushirika ni kuinua na kuimarisha hali ya kiuchumi na kijamii ya wanachama wake (Vijana) kwa kufuata kanuni na taratibu za vyama vya ushirika. Hivyo basi napenda kutoa wito kwa vijana wote wa manispaa ya Musoma kujiunga na Chama hiki. Vijana Musoma SACCOS ni kwa Ajiri ya Maendeleo yako Binafsi, Familia yako, Jamii yako, na Taifa kwa Ujumla”.
“Weka Akiba Mara kwa Mara, Kopa kwa Busara, Lipa Upesi”

MAUAJI YA KIKATILI DHIDI YA WANAWAKE KUENDELEA MKOANI MARA



Kulia juu ni picha ya mwili wa marehemu Nyamata Gwanumbu Monda Nyamsha, na ya pili ni maafisa wa polisi wakishusha mwili wa mareheu nyumbani kwao Kiemba Nyakatende.

Mama mmoja aliyefahamika kwa majina ya Nyamata Gwanumbu Monda Nyamsha, mwenye umri wa miaka iliyokadiriwa 38, watoto 5. Mkazi wa Mkoa: Mara, Wilaya: Butiama, Kata: Nyakatende, Kijiji: Kiemba. Tarehe 10 April, 2014 Saa 3 Asubuhi alikutwa shambani kwake akiwa mauti na amezikwa kwa kufukiwa kwa udongo chini ya kichaka kilichoko shambani kwake, hata hivyo marehemu alikutwa ana jereha la kupigwa kichwani eneo la kisogoni.


Kisa Mkasa
Marehemu asubuhi aliwahi kuamka na kuelekea shambani kwake kuchimba viazi huku akiwa amewaachia watoto wake maagizo ya kuja saa 3 asubuhi shambani hapo kumpokea viazi atakavyokuwa amechimba. Mda huo ulipofika watoto wa marehemu walikwenda shambani kufuata viazi kama marehemu mama yao alivyokuwa amewaambia.  Walipofika shambani hawakumuona marehemu mama yao ndipo walianza kuita mama mama……, ghafla walimuona mtu (mwanamume) akitoka kichakani akiwa uchi kama alivyozaliwa akiwa na panga mkononi, walikimbia wakipiga kelele.  Ndipo wananchi walipojitokeza kujua kulikoni. Katika zoezi la kumtafuta mama huyo ndipo alipokutwa kichakani hapo akiwa ameuwawa.
Kwa mujibu wa Mhe. Diwani wa kata ya Nyakatende Ndg.Kasonyi mauaji hayo ni mauaji ya nne(4) tangu mauaji hayo yaanze kuzuka wilani Butiama, Mugango mauaji mara mbili (2), yakiongozwa na Nyegina mauaji mara nane (8)

Tarehe 22/03/2014 saa 2 Asubuhi  yalitokea mauaji mengine pia ya mama aliyefahamika kwa majina ya Yasinta Kate Matiku kwa kabila Mkwaya, miaka 34, na familiya ya watoto 2. Mkazi wa Kijiji cha Kamguruki, Kata ya Nyakatende, Tarafa ya Nyanja, Wilaya ya Butiama, mkoani Mara.

Kisa Mkasa
Asubuhi ya saa 2 marehemu aliondoka nyumbani kwenda kununua vitumbua gengeni(Center), ndiko alipokutwa na mauaji hayo. Mwili wake ulikuwa unajeraha kupigwa na kitu chenye incha kali, kisha kumwagiwa maji ya moto sehemu za mapajani, mgongoni na mbavuni, mkanda wa suruali shingoni na ukiwa umeondolewa baadhi ya viungo vyake vya siri (maalufu kwa jina la Memory card)
Ukiwa mzalendo na mpenda Amani unashauri nini kifanyike………………………….?, Toa maoni yako ili kutokomeza mauaji haya yanayoendelea.

TANLAP YATOA MAFUNZO YA WATU WENYE ULEMAVU NA USULUHISHI MBADALA WA MIGOGORO

Saturday, March 29, 2014



Mtandao wa watoa msaada wa kisheria (TANZANIA NETWORK OF LEGAL AID PROVIDERS-TANLAP) inaendesha mafunzo ya sheria ya watu wenye ulemavu na usuluhishi mbadala wa migogoro, kwa wanachama wake wapatao 60. Mafunzo yamefanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 27/3/2014 hadi 29/3/2014 katika Hotel ya Tamal jijini Dar es Salaam.
ü  Siku ya Kwanza: 27/3/2014: Sheria ya Watu wenye Ulemavu
ü  Siku ya Pili: 28/3/2014: Utatuzi wa Migogoro Kutumia Njia Mbadala
ü  Siku ya Tatu:  29/3/2014: Utatuzi Mbadala ya Migogoro
Bwn. Gideoni Mandesi (Wakili), kama mwezeshaji wa mafunzo sheria ya watu wenye ulemavu akifafanua Sheria Na. 9 ya mwaka 2010 alieleza makundi 7( Upofu, viungo, akili, kiziwi, ulemavu wa ngozi, , uono hafifu na ulemavu wa viungo) ya walemavu na kusisitiza kwamba pamoja na uwepo wa sheria hii Asasi za kiraia zina wajibu kisheria wa kufanya ili sheria hii iwasaidie walengwa, na kusisitiza misingi ya sheria hii (Kifungu cha 4. (a)-(g) kama ifuatavyo.
a)      Kuheshimu utu, uhuru wa mtu
b)      Kutobaguliwa
c)       Kushurikishwa katika nyaja zote katika jamii
d)      Usawa wa fursa
e)      Ufikikaji
f)       Usawa wa kijinsia kwa kutambua haki na mahitaji ya walemavu
g)      Kutoa usalama na ulinzi wa kijamii

Adhabu kwa Unyanyapaa wa Walemavu
1)      Kwa taasisi; faini isiyo chini ya shilingi millioni mbili(2,000,000/=)  na isiyopungua shilingi million ishirini (20,000,000/=)
2)      Kwa mtu binafsi; faini isiyopungua shilingi laki tano (500,000/=) na isiyozidi shilingi milioni saba(7,000,000/=) au
Kufungwa jela mwaka mmoja au vyote kwa pamoja
Bwn James Marenga (wakili), mwezeshaji wa usuluhishi mbadala wa migogoro. Alitoa hatua 7 za ukuaji wa migogoro
1)      Kutokuwepo taarifa na takwimu sahihi
2)      Mahusiano
3)      Thamani
4)      Muundo
5)      maslahi
Aidha alisisitiza ni vizuri na muhimu sana kila sahuli lipitie hatua ya  usuluhishi mbadala wa migogoro kabla ya shauri hilo kwenda kwenye ngazi za mahakama na sheria inalitambua hilo na kulipa uzito. na kuwataka washiriki hao ambao ni wanachama wa mtandao huo kutumia njia mbadala wa usuluhishi wa migogoro kabla ya mashauri hayo kwenda mahakamani akibainisha na faida zake katika tathnia ya sheria.

Followers

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. TZ Youth Potentials - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Inspired by Sportapolis Shape5.com
Proudly powered by Blogger