SERA YA TAIFA YA MAENDELEO YA VIJANA
Sera hii
iliandaliwa kwa ajili ya kusimamia maslahi ya kijana, ambayo serikali iliandaa
mwaka 1996 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2007
Sera ya taifa ya
maendeleo ya vijana ya 2007 inalenga masuala ya maendeleo ya vijana ambayo ni
pamoja na: uwezeshaji wa kiuchumi, mazingira, VVU na Ukimwi, jinsia, sanaa na
utamaduni, michezo afya ya uzazi kwa vijana na masuala ya maisha ya familia.
LENGO LA SERA
- Kuhakikisha taifa linakuwa na vijana wenye uwezo, wenye ari ya kutosha , wawajibikaji na wanaoshiriki kikamilifu katika Nyanja zote za kijamii, kisiasa na kiuchumi kwa maendeleo ya jamii.
- Kuweka mazingira yanayowezesha kujenga uwezo wa vijana na kukuza nafasi za ajira na kupata huduma ya hifadhi ya jamii
Kwa kifupi lengo
ni kuwajengea uwezo, kuwawezesha na kuwaongoza vijana na wadau wenginekatika
utekelezaji wa masuala ya maendeleo ya vijana
Sera ya taifa ya
vijana imeandaliwa ili sisi vijana wa kike na wa kiumetuendelee kuleta msukumo
wawa kuleta mageuzi ya kijamii, kiuchumi na kisiasa katika eneo lenye
mabadiliko ya haraka duniani.
Maendeleo yetu
ya kijamii yanategemea, pamoja na vitu vingine, ni kwa jinsi gani vijana
tunahusika katika kujenga maisha ya baadaye. Hivyo ni kwa sababu hii sera
inatuandaa kuwa viongozi, watoa uamuzi, wajasiriamali, wazazi na walezi kwa
sababu tuna nafasi muhimu katika maendeleo ya jamii na uchumi wa taifa letu.
Sera ya taifa ya
vijana imetoa maelekezo kwa vijana, washirikiane na wadau wengine katika
masuala ya maendeleo yetu. Ila sera ni muongozo tu, utekelezaji wake ndio utakao tuwezesha kuvuna matunda ya sera hii
nzuri .hatuna budi kuijua na kusimamia utekelezaji wake kwenye Nyanja
mbalimbali kuanzia kwenye maeneo tunayoishi hadi serikali kuu
Wadau wote
tushirikiane katika kutekeleza sere hii, hakika tutatengeneza vijana
watakaolipeleka taifa hili mbele kimaendeleo (fema, APRIL-JUNE 2013.ONE DAY YES!, Youth POWER!, Zungumza na
Mwanafunzi. Uk wa 2)
You actually make it seem so easy with your presentation but I find this topic to
ReplyDeletebe really something that I think I would never understand. It seems
too complicated and extremely broad for me.
I'm looking forward for your next post, I'll try to get the hang
of it!
weka document ya sera ya vijana humu tuweze kuipakua, swahili version
ReplyDelete