Simanzi
na majozi vimeendelea kuikumba jamii ya mkoani Mara baada ya kuzuka Mauaji ya
kikatili ya kuchinja vichwa kwa wanawake, kunyongwa na hata kuondolewa sehemu
zao za siri ikiwa ni pamoja na kutobolewa macho kuendelea kushamili na kuifanya
Haki ya Kusishi kubaki kuwa kitendawili kwa wanawake mkoani Mara hususani
wilaya ya Butiama na Musoma. Mauji haya tangu kuzuka yapata ni mwaka mmoja sasa
(tangu 2013) na ufumbuzi wake ni sitofahamu.
Mama mmoja kwa jina Nyasatu Paulo
mwenye umri wa miaka 24, mkazi wa kijiji cha Kigera Etuma, Kata ya Nyakatende,
Tarafa ya Nyanja, Wilayani Butiama-Mara, alikutwa mauti shambani kwake kwa kifo
cha kunyongwa shingo na kisha kifukiwa kwa udongo wa matuta kama mzoga. Marehemu
alipotea siku moja kabla (tarehe 30/01/2014 Alihamisi) ya kupatikana mashambani
akiwa mauti (tarehe 31/01/2014 Ijumaa). Marehemu ameacha familia ya mume na
watoto 3, mdogo ( mtoto wa tatu) akiwa mwenye umri wa miezi 8.
Wanainchi
wenyeji wa maeneo ambamo mauaji haya hutokea wanabaini kuwa mauji haya
yanatokana na sababu kuu mbili:1. Imani za kishirikina, na ya 2. Visasi. Eidha
walibainisha kuwa Haki ya Usawa kwa wanawake pia imekuwa ndoana kwa wale
wanaodhubutu kuisimamia na kuidai hususani kumiliki au kurithi rasilimali mfano
ardhi, ng’ombe na nyumba.
Wanainchi
wameendelea kuitupia serikali lawama kuwa haijaamua kutokomeza mauaji haya ya
kikatili kwa wanawake yanayoendelea mkoani Mara. “Kama wanyamapori wanakufa na
Serikali inaanzisha Oparesheni Tokomeza kuzuia mauaji ya wanyamapori/Majangiri,
Je binadamu si rasilimali ya Taifa, mpaka ione haja ya kuwepo na Oparesheni ya
kutokomeza mauaji haya…?, Ni ajabu serikali yetu kuliacha swala hili kwa sehemu
kubwa mikononi mwa wanainchi!” Alisema Mkazi wa Kijiji cha Kigera Etuma kwa
Uchungu.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !