Umma wa watanzania wanaharakati wa kupinga vitendo vya Ukatili wa Kijinsia jumanne tarehe 25, Novemba 2014 watazindua kampeni hii kitaifa, kimkoa na maeneo mbalilmbali ya kiutendaji. Hii ni kampeni ya siku 10 na huzinduliwa tarehe 25, Novemba ya kila mwaka hadi tarehe 10, Desemba.
Kitaifa itazinduliwa pale Viwanja vya Karimjee
kuanzia saa 3 asubuhi. Uzinduzi huu utafuatana
na maandamano ya amani yakihamasisha jamii kuachana na Vitendo vya
Ukatili wa Kijinsia, kuanzia viwanja vya mnazi mmoja kupitia, barabara ya Morogoro,
barabara ya Bibi Titi Mohamed, Ali Hassan Mwinyi,Mtaa wa Ohio, Samora hadi
Viwanja vya Karimjee. Yote haya yataanza saa 1:30 asubuhi.
Kauli Mbiu ya mwaka huu ni “FUNGUKA! FICHUA UKATILI WA KIJINSIA KWA AFYA YA JAMII” ,Katika Kiingereza, “OPEN UP! DISCLOSE GENDER BASED VIOLENCE FOR THE HEALTH OF THE COMMINITY”
Kauli Mbiu ya mwaka huu ni “FUNGUKA! FICHUA UKATILI WA KIJINSIA KWA AFYA YA JAMII” ,Katika Kiingereza, “OPEN UP! DISCLOSE GENDER BASED VIOLENCE FOR THE HEALTH OF THE COMMINITY”
Kampeni
hii kitaifa inaratibiwa na Shirika na WiLDAF kwa kushirikiana na Wadau toka
Irish AID na UN Women.
Watanzania
tupinge Vitendo vyote vya Ukatili wa Kijinsia, vitendo hivi huongeza mzigo kwa
maendeleo ya jinsi zote, familia, jamii husika na taifa kwa ujumla.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !