Kikundi
cha TUNAWEZA ni ushirika wa hiari wa ujasiriamali wa
kilimo, ufugaji na biashara kwa maendeleo ya wanakikundi, kikundi, jamii na
taifa kwa ujumla. Kikundi hiki kipo Mtaa wa Kiara, Kata ya Kigera, Manispaa ya
Musoma.
Katibu wa kikundi, Japheth M. Kurwa alisema yafuatayo “Tunaimani
juu ya kilimo, na kwa sasa tunayo miradi miwili ya kilimo; wa kwanza ni mradi
wa kilimo cha Mhogo katika eneo la Kisiwani-Kiara lililoko wilayani Manispaa ya
Musoma, na kwa mradi huu tunazo ekari 5, na mradi wa pili ni kilimo cha zao la biashara
la mahindi, katika eneo la bonde la mto Suguti lililoko wilayani Bunda mkoani
Mara. Tunazo hekari 15 za mahindi tutakazolima msimu.
Miradi yote hii tunajikita
katika kuzalisha katika hali ya ubora na ufanisi ili kupunguza balaa la njaa
katika jamii na kwa taifa kwa ujumla, ikiwa ni pamoja na wanakikindi kujiajiri
katika kilimo.
Pamoja na jitihada zote
hizi katika kilimo bado tunakabiliwa na changamoto ya ukosefu mitaji ili tuweze
kuwekeza na kuzalisha kwa ufanisi mkubwa. Tunaupungufu wa pembejeo za kilimo na
nyenzo za kisasa ambayo huadhili miradi hii kwa kiasi kikubwa.
Changamoto ya pili ni ya
mabadiliko ya tabia nchi, hii inatulazimu kununua machine za umwagiliaji kwani
mvua sasa ni tatizo.
Kama kikundi tunayo mikakati madhubuti
ya kuweza kupata mikopo na kwa sasa tumekwisha omba toka Halmashauri ya
Manispaa ya Musoma kupitia fedha za vijana-Katani kufadhili mradi wa kilimo cha
Muhogo, pia temeomba fedha toka Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo kupitia
mfuko wa maendeleo ya vijana. Lakini pia wanakikundi tunao utaratibu wa
kuchangia miradi hii. Mwenyezi Mungu akitujaharia kupata fedha hizi tunaamini
kupitia kilimo tutafanya mambo makubwa.
Si sahihi kuwa na dhana kwamba kilimo
cha biashara kinaweza kufanywa na watu wenye kipato cha kati na cha juu.
Tumeanza mwaka jana miradi yote hii na sasa tumeona kuwa inawezekana na
TUNAWEZA kwani wazo tunalo, watu tunao na kwa umoja wetu tutaujenga uchumi
wetu”.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !