CHAMA CHA USHIRIKA
CHA AKIBA NA MIKOPO CHA VIJANA MUSOMA SACCOS (VIMU SACCOS) LTD
S.L.P …., Musoma-Mara. Simu: 0756290672, 0755671818, & 0654655498
S.L.P …., Musoma-Mara. Simu: 0756290672, 0755671818, & 0654655498
Vijana wapatao 45, manispaa ya
Musoma wameazimia kuunda na kusajiri Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo
kijulikanacho kwa jina la VIJANA MUSOMA SACCOS LTD kwa lengo la kuinuana khali
zao kiuchumi na kijamii.
Mwenyekiti wa Bodi ya uanzilishi
wa Chama hicho, Bwn. Japheth M. Kurwa; alisema “Wanachama wa chama cha ushirika
cha VIJANA MUSOMA SACCOS (VIMU SACCOS) tumeamua rasmi na kwa dhati
kusaidiana, kushirikiana, kuthaminiana, kujaliana, kujiendeleza na kusimamia
ubora wa maisha yetu ili kila mmoja apate unafuu na furaha katika maisha kwa
kuzingatia misingi ya uhuru, haki, udugu na amani, Madhumuni ya chama hiki
cha ushirika ni kuinua na kuimarisha hali ya kiuchumi na kijamii ya wanachama
wake (Vijana) kwa kufuata kanuni na taratibu za vyama vya ushirika. Hivyo basi napenda kutoa wito kwa vijana wote
wa manispaa ya Musoma kujiunga na Chama hiki. Vijana Musoma SACCOS ni
kwa Ajiri ya Maendeleo yako Binafsi, Familia yako, Jamii yako, na Taifa kwa Ujumla”.
“Weka Akiba
Mara kwa Mara, Kopa kwa Busara, Lipa Upesi”
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !