MAENDELEO YA VIJANA: TUNAO WAJIBU WA KUFANYA

Thursday, October 16, 2014

Utangulizi
  Changamoto ya maendeleo ya vijana ni suala mtambuka. Uwezeshaji wa vijana unajumuisha juhudi za pamoja za wadau mbalimbali muhimu pamoja na serikali, jamii, sekta binafsi, asasi za kijamii, familia na vijana wenyewe.
  Kwa mujibu wa sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007; vijana fasili yake ni Vijana wa kiume na kike kuanzia umri wa miaka 15 hadi 35.
Wadau wa Maendeleo ya Vijana
Wadau wa maendeleo ya vijana ni pamoja na:-
  • Serikali
  • Jamii
  • Sekta binafsi
  • Asasi za kijamii
  • Familia
  • Vijana wenyewe
Kada, Ofisi, Idara na Taasisi za Umma Zinazoshughulika moja kwa moja na Masuala/ Maendeleo ya Vijana
  Kada/ofisi ya Maendeleo ya Vijana; inaratibu masuala yote ya vijana
  Kada/ofisi ya Utamaduni
  Kada/ofisi ya Michezo
  Kada/ofisi ya Maendeleo ya Jamii; kwa usajiri wa Vikundi
  Kada/ofisi ya Ushirika; ushauri wa kitaalam na kisheria kuhusu ushirika wa vikundi kama vile SACCOS, VICOBA n.k na Usajili
  Idara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana
  VETA
Fursa za Vijana toka Serikalini
  Mfuko wa Taifa wa Maendeleo ya Vijana; unatoa mikopo kwa vikundi vya maendeleo ya vijana nchini kote kupitia SACCOS za Vijana zinazoendelea kuudwa na vijana wenyewe kila halmashauri nchini
  Mradi wa kufyatua Tofari wa Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) kwa halimashauri zote nchini
  Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF); unatoa mikopo ya mitaji kwenye SACCOS zikiwemo zile za Vijana
  Halmashauri; zina mfuko wa kukopesha/ kuwawezesha vikundi vya wanawake na vijana kupitia ofisi ya mtendaji wa kata na Kamati za Maendeleo ya Kata(WDC) n.k
Wosia kwa Vijana na Wadau wa Wamaendeleo ya Vijana
  Taifa halimuangalii kijana kama tatizo bali kama rasilimali na nguvukazi ya kujenga uchumi wa Taifa
  Taifa linatambua ushindani mkubwa wa kimaendeleo baina ya vijana na ubunifu walionao
  Kuna kila haja ya kuwekeza zaidi katika ubunifu wa vijana (Youth initiatives) ili waweze kujiajiri na kuajiri vijana wenzao.
  Tunao wajibu wakufanya; ikiwa ni pamoja na kuchangamkia fursa zote za maendeleo na kuzitumia vizuri.
  Kwa changamoto ya mitaji inayotukabili vijana; tukumbuke umoja ni nguvu  hivyo yatupasa kuunda/ kuanzisha ushirika ili kuweza kupata mitaji
  Vijana wengi hawana mahusiano mazuri na sekta rasmi, hivyo kila mdau atambue anao wajibu wa kufanya ili kusaidia suala la maendeleo ya vijana; hususani kijana mwenyewe

Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Followers

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. TZ Youth Potentials - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Inspired by Sportapolis Shape5.com
Proudly powered by Blogger