Songea.
Vilio na simanzi vimetawala katika baadhi ya familia za askari wa Jeshi
la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambao waliuwawa katika eneo la Darfur,
Sudan ambako wanashiriki katika ulinzi wa amani.
Mamia ya waombolezaji
walionekana katika makazi ya familia za marehemu; Songea mkoani Ruvuma
na Nachigwea mkoani Lindi ambako ziko kambi ambazo baadhi ya askari hao
walikuwa wakifanya kazi.
Imefahamika kuwa wanajeshi
waliouwawa Jumamosi iliyopita wanatoka katika vikosi vya, 42KJ Chabruma,
Songea, 44KJ Mbeya, 36KJ Msangani, 92KJ Ngerengere, 94KJ cha Mwenge,
Dar es Salaam, 41KJ Nachingwea na Makao Makuu ya JWTZ- Upanga, Dar es
Salaam.
Jana gazeti hili lilibaini
kuwapo kwa maombolezo katika baadhi ya familia za wanajeshi hao baada ya
kupokea taarifa za vifo vyao kutoka JWTZ. Hata hivyo bado majina ya
waliofariki hayajawekwa hadharani.
Msemaji Mkuu wa JWTZ, Kanali
Kapambala Mgawe juzi aligoma kutaja majina hayo akisema kuwa majina hayo
hayajatolewa rasmi na kwamba familia za marehemu zilikuwa
hazijajulishwa.
“Hayo majina yanayotajwa kwenye
mitandao ni ya uongo. Kwa sasa mimi sijaletewa majina na utaratibu
uliopo ni hadi ‘next of kin’ (ndugu) wao wajulishwe kwanza,” alisema
Kanali Mgawe.
Hata hivyo kupitia katika maeneo
ilikokuwa misiba hiyo jana, gazeti hili lilifanikiwa kufahamu majina ya
baadhi yao, ambayo yanafanana na yale yaliyotangazwa kwenye mitandao ya
kijamii pamoja na baadhi ya magazeti.
Katika Kambi ya Chabruma, Songea
mkoani Ruvuma kulikuwa na umati wa waombolezaji nyumbani kwa mmoja wa
wapiganaji hao, Koplo Oswald Chaula ambaye alikuwa katika Kikosi cha
Mizinga Chabruma na ndugu zake walikiri kupokea taarifa za msiba huo.
Hali kama hiyo ilikuwa nyumbani
kwa Koplo Mohamed Chukilizo katika Kambi ya Majimaji, Nachingwea ambako
baadhi ya ndugu na jamaa za zake wakiwamo mkewe na baba mkwe wake
walikutana jana jioni kujadiliana kuhusu msiba.
Mwananchi pia lilishuhudia
waombolezaji wakiwa wamekusanyika eneo la Mjimwema, Songea Mkoani Ruvuma
ambako ni nyumbani kwa Komandoo Rodney Ndunguru aliyetoka kikosi cha
92KJ Ngerengere, Morogoro, baada ya kupokea taarifa za msiba huo.
Vilio, Simanzi
Katika kambi ya Chabruma, mke wa
marehemu Koplo Oswald aliyejitambulisha kwa jina la Maria alikuwa
akilia kwa simanzi baada ya kupata taarifa kuwa miongoni mwa waliofariki
ni baba watoto wake.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !