TANLAP YATOA MAFUNZO YA WATU WENYE ULEMAVU NA USULUHISHI MBADALA WA MIGOGORO

Saturday, March 29, 2014



Mtandao wa watoa msaada wa kisheria (TANZANIA NETWORK OF LEGAL AID PROVIDERS-TANLAP) inaendesha mafunzo ya sheria ya watu wenye ulemavu na usuluhishi mbadala wa migogoro, kwa wanachama wake wapatao 60. Mafunzo yamefanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 27/3/2014 hadi 29/3/2014 katika Hotel ya Tamal jijini Dar es Salaam.
ü  Siku ya Kwanza: 27/3/2014: Sheria ya Watu wenye Ulemavu
ü  Siku ya Pili: 28/3/2014: Utatuzi wa Migogoro Kutumia Njia Mbadala
ü  Siku ya Tatu:  29/3/2014: Utatuzi Mbadala ya Migogoro
Bwn. Gideoni Mandesi (Wakili), kama mwezeshaji wa mafunzo sheria ya watu wenye ulemavu akifafanua Sheria Na. 9 ya mwaka 2010 alieleza makundi 7( Upofu, viungo, akili, kiziwi, ulemavu wa ngozi, , uono hafifu na ulemavu wa viungo) ya walemavu na kusisitiza kwamba pamoja na uwepo wa sheria hii Asasi za kiraia zina wajibu kisheria wa kufanya ili sheria hii iwasaidie walengwa, na kusisitiza misingi ya sheria hii (Kifungu cha 4. (a)-(g) kama ifuatavyo.
a)      Kuheshimu utu, uhuru wa mtu
b)      Kutobaguliwa
c)       Kushurikishwa katika nyaja zote katika jamii
d)      Usawa wa fursa
e)      Ufikikaji
f)       Usawa wa kijinsia kwa kutambua haki na mahitaji ya walemavu
g)      Kutoa usalama na ulinzi wa kijamii

Adhabu kwa Unyanyapaa wa Walemavu
1)      Kwa taasisi; faini isiyo chini ya shilingi millioni mbili(2,000,000/=)  na isiyopungua shilingi million ishirini (20,000,000/=)
2)      Kwa mtu binafsi; faini isiyopungua shilingi laki tano (500,000/=) na isiyozidi shilingi milioni saba(7,000,000/=) au
Kufungwa jela mwaka mmoja au vyote kwa pamoja
Bwn James Marenga (wakili), mwezeshaji wa usuluhishi mbadala wa migogoro. Alitoa hatua 7 za ukuaji wa migogoro
1)      Kutokuwepo taarifa na takwimu sahihi
2)      Mahusiano
3)      Thamani
4)      Muundo
5)      maslahi
Aidha alisisitiza ni vizuri na muhimu sana kila sahuli lipitie hatua ya  usuluhishi mbadala wa migogoro kabla ya shauri hilo kwenda kwenye ngazi za mahakama na sheria inalitambua hilo na kulipa uzito. na kuwataka washiriki hao ambao ni wanachama wa mtandao huo kutumia njia mbadala wa usuluhishi wa migogoro kabla ya mashauri hayo kwenda mahakamani akibainisha na faida zake katika tathnia ya sheria.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Followers

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. TZ Youth Potentials - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Inspired by Sportapolis Shape5.com
Proudly powered by Blogger