Kulia juu ni picha ya mwili wa marehemu Nyamata Gwanumbu Monda Nyamsha, na ya pili ni maafisa wa polisi wakishusha mwili wa mareheu nyumbani kwao Kiemba Nyakatende.
Mama mmoja aliyefahamika kwa
majina ya Nyamata Gwanumbu Monda Nyamsha, mwenye umri wa miaka iliyokadiriwa
38, watoto 5. Mkazi wa Mkoa: Mara, Wilaya: Butiama, Kata: Nyakatende, Kijiji:
Kiemba. Tarehe 10 April, 2014 Saa 3
Asubuhi alikutwa shambani kwake akiwa mauti na amezikwa kwa kufukiwa kwa udongo
chini ya kichaka kilichoko shambani kwake, hata hivyo marehemu alikutwa ana
jereha la kupigwa kichwani eneo la kisogoni.
Kisa Mkasa
Marehemu asubuhi aliwahi kuamka
na kuelekea shambani kwake kuchimba viazi huku akiwa amewaachia watoto wake
maagizo ya kuja saa 3 asubuhi shambani hapo kumpokea viazi atakavyokuwa
amechimba. Mda huo ulipofika watoto wa marehemu walikwenda shambani kufuata
viazi kama marehemu mama yao alivyokuwa amewaambia. Walipofika shambani hawakumuona marehemu mama
yao ndipo walianza kuita mama mama……, ghafla walimuona mtu (mwanamume) akitoka
kichakani akiwa uchi kama alivyozaliwa akiwa na panga mkononi, walikimbia
wakipiga kelele. Ndipo wananchi
walipojitokeza kujua kulikoni. Katika zoezi la kumtafuta mama huyo ndipo
alipokutwa kichakani hapo akiwa ameuwawa.
Kwa mujibu wa Mhe. Diwani wa kata
ya Nyakatende Ndg.Kasonyi mauaji hayo ni mauaji ya nne(4) tangu mauaji hayo
yaanze kuzuka wilani Butiama, Mugango mauaji mara mbili (2), yakiongozwa na
Nyegina mauaji mara nane (8)
Tarehe 22/03/2014 saa 2 Asubuhi
yalitokea mauaji mengine pia ya mama aliyefahamika kwa majina ya Yasinta
Kate Matiku kwa kabila Mkwaya, miaka 34, na familiya ya watoto 2. Mkazi wa
Kijiji cha Kamguruki, Kata ya Nyakatende, Tarafa ya Nyanja, Wilaya ya Butiama,
mkoani Mara.
Kisa Mkasa
Asubuhi ya saa 2 marehemu
aliondoka nyumbani kwenda kununua vitumbua gengeni(Center), ndiko alipokutwa na
mauaji hayo. Mwili wake ulikuwa unajeraha kupigwa na kitu chenye incha kali,
kisha kumwagiwa maji ya moto sehemu za mapajani, mgongoni na mbavuni, mkanda wa
suruali shingoni na ukiwa umeondolewa baadhi ya viungo vyake vya siri (maalufu
kwa jina la Memory card)
Ukiwa mzalendo na mpenda Amani
unashauri nini kifanyike………………………….?, Toa maoni yako ili kutokomeza mauaji haya
yanayoendelea.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !