Katika juhudi zetu za
kuleta maendeleo ya vijana, jamii na taifa kwa ujumla; na kugusa mahitaji muhimu , ni lazima kukumbuka kwamba binadamu ni wa muhimu zaidi ya mahitaji
yake, na muhimu zaidi katika hili ni kuifanya jamii ijiletee maendeleo yake
inayoyahitaji. Hivyo wadau wa maendeleo, serikali ikiwa mstali wa mbele ni
kuweka mazingira rafiki kwa maendeleo. Mazingira haya ni yale halisi mfano:
rasilimali na mazingira ya nadharia mfano: mazingira ya kijamii, kisiasa,
kichumi na kitamaduni.
Ni jambo la kusikitisha
sana kwa siasa za Tanzania ya leo, kwani
zinakampeni ya kulenga mahitaji ya watu zaidi kuliko watu wenyewe. Vijana
na watanzania wote kwa ujumla tuweni welevu na wenye busara juu ya mustakabali
mzima wa siasa na wanasiasa. Napenda kutoa wito kwa watanzania wote hasa
vijana, tuwe na tafakari ya kina na kuchukua hatua. Nipo kwenye mkakati wa
kuwaandikia watanzania kijarida chenye kichwa cha habari “WATANZANIA TUJITATHMINI NA SIASA ZETU” humo nitazungumza mengi juu
ya mwenendo wa siasa ya leo na madhara yatokanayo. Alisema Bw. Japheth M. Kurwa-Mkurugenzi wa TYPs-ASSOCIATION
katika ofisi za Asasi hiyo ya maendeleo ya Vijana zilizoko ndani ya kituo cha Matumaini
katika Vijana-Manispaa ya Musoma, tarehe 08/08/2013
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !