Kundi
hili ni kundi linalojumuisha vijana wengi zaidi kuliko lile la vijana wasomi.
Vijana wengi walioko katika kundi hili ni wale walioko katika ajira zisizo
lasmi kama vile; uvuvi, kilimo, kubeba
mizigo, ufugaji, machinga, garage, udereva wa magari na pikipiki (Bodaboda),
ulinzi, vibarua vya ujenzi, vibarua katika sekta ya madini, migahawa/ vibanda
vya lishe na kuchoma chips, saloon, uselemala, vibarua viwandani n.k
1.
Tafsiri
Baadhi ya Maneno
Ajira: Ni shughuli yoyote halali (rasmi au
isiyo rasmi), inayomwezesha mwananchi kujipatia riziki, mahitaji na kipato cha
kuendesha maisha yake, ya familia na pengine kuchangia katika pato la eneo
alipo au Taifa.
Kutokuwa
na ajira: Ni hali ya kukosa kazi kabisa au nguvukazi iliyopo
kutotumika kuzalisha mali au kutoa huduma.
Kijana: Zipo tafsiri aina mbili;
i)
Kimataifa; Kijana ni mtu mwenye umri wa
miaka 15 hadi 24
ii)
Kwa Tanzania ni miaka 15 hadi 35
Sekta
isiyo rasmi: Hii ni sekta ambayo si ya shambani wala
ofisini, ya kiwango cha chini na ya kujiajiri inayotumia mtaji na teknolojia ndogo.
Fursa: Ni
shughuli za kiuchumi na kijamii au za uzalishaji mali au huduma ambazo
hutekelezwa na mtu na kuweza kumpatia kipato halali.
2.
Fursa
ya Uvuvi na Uzaji wa Samaki-Kisiwani Lukuba
Sekta
ya Uvuvi ni moja ya sekta iliyoajiri vijana wengi hapa Tanzania, Kisiwa cha
lukuba ni moja ya Visiwa vilivyoko mkoani Mara chenye fursa kubwa ya ajira ya
kujiajiri.
Kisiwa
hiki kinatoa fursa nyingi za ajira ya kujiajiri kwa vijana hususani wale ambao
hawakubahatika kwendelea na masomo. Fursa za ajira ni uvuvi unaoambatana na usafirishaji,
uchakataji, uchuuzi wa samaki na uzalishaji viwandani, ujenzi wa mitumbwi/boti
za uvuvi.
Kisiwa
hiki kinategemea shughuli ya uvuvi na uuzaji wa samaki hususani samaki aina ya Dagaa na Sangara
(Nile perch). Uvuvi katika kisiwa hiki unatoa mchango mkubwa katika kuinua
kiwango cha maisha ya vijana hawa, wananchi wa Musoma na nchi kwa ujumla. Hata hivyo, fursa bado ni kubwa kwa
wawekezaji wengi kuwekeza katika eneo hili.
Serikali
inatakiwa kuongeza juhudi za makusudi kuhakikisha uendelevu wa raslimali ya
uvuvi ambayo ni msaada mkubwa kwa taifa. Aidha inatakiwa kuliangalia eneo hili
kwa makini ili kuwawezesha vijana hususani kundi hili ambalo halikubahatika
kuendelea na masomo yao.
3. Changamoto
ya Jumla Kuhusu Ajira ya
Vijana ambao Hawakubahatika Kuendelea na Masomo.
Kundi
hili ni kundi linalojumuisha vijana wengi zaidi kuliko lile la vijana wasomi, kwa mtazamo wa haraka kundi hili la
vijana ni kama limesahulika.; changamoto zinazolikabili kundi hili
ni pamoja na:-
·
Hali ya kutokuwa na fursa ya kushiriki
katika uchumi inayosababishwa na uwezo mdogo katika mitaji, ukosefu wa ujuzi na
uzoefu wa biashara, pamoja na matatizo yanayohusiana na kutokopesheka.
·
Hali ya kutopata fursa ya kushiriki katika fursa
za kiuchumi katika mfumo rasmi
·
Kutopokelewa na jamii katika mtazamo chanya;
kunakoleta tafasili kandamizi kwao kama vile tafasiri ya wahuni na watu
waliofeli maisha, tafasili ambayo hupelekea vijana hao kuwa hivyo.
·
Uhusiano mdogo wa kundi hili na sekta rasmi,
taasisi binafsi na za umma; na Serikali kwa ujumla
4. Nini
Kifanyike
Wadau
wote wa maendeleo ya vijana (serikali, jamii, sekta binafsi, Asasi za kijamii,
familia na vijana wenyewe) kuwa karibu sana na kundi hili kama walezi na walimu; na kutekeleza wajibu huu ipasavyo
Vijana
kuchangamkia fursa na kuzitumia ipasavyo katika kuwekeza na kuzalisha (Saving
and Production). Ogopeni semi kama vile: Tumia pesa ikuzoee, elfu moja
haijengi, raha jipe mwenyewe, kula ujana maisha yenyewe mafupi n.k
Maeneo
haya yenye kuwaajiri vijana walioko katika kundi hili, yakipewa kipaumbile na
kutengenezwa kuwa mazingira rafiki ya kujiajiri yatapunguza kwa kiasi kikubwa
kero ya ajira kwa vijana na taifa kwa ujumla.
By:
Mr. Japheth M. Kurwa
Falsafa
yangu ni:- “JUHUDI ZISIZOKOMA KATIKA KUJIFUNZA NA KUFANYA KAZI”
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !