Pichani
ni viongozi wa vikundi vya maendeleo ya vijana (vikundi 31) kutoka wilaya za
Butiama na Musoma wakiwa na maafisa wa serikali na Asasi za kiraia katika picha
ya pamoja ndani ya viwanja vya Kituo cha Matumaini katika Vijana-Manispaa ya
Musoma
Maafisa hao ni
pamoja na: Ndugu Adolfu Kami wa kwanza kushoto waliosimama mstari wa kwanza,
afisa maendeleo ya vijana manispaa ya Musoma, ndugu Masatu Rugee, afisa michezo
na utamaduni halimashauli ya wilaya ya Musoma, Afisa utawala na Fedha Ndugu
Robert Moro, wa Shirika la Kutetea Haki za Wanawake na Watoto (ABC FOUNDATION);
na Ndugu George Muyabi mratibu wa Mara Development Forum (MDF), pamoja na afisa
mmoja wa CHODAWU na Idara ya Kazi na Ajira-Musoma
Asasi
iliwakutanisha viongozi wa vikundi vya maendeleo ya vijana (vikundi 31) na
maafisa hao kwa lengo la vijana hao kutambua fursa na wajibu wao ili waweze
kunufaika na fursa zilizo katika ofsi za idara hizo za serikali
“Kila kijana ni
muhimu kutambua haki na wajibu wake; kila kijana ana haki na wajibu wa
kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo yake bifsi, ya jamii pamoja
na taifa kwa ujumla. Na kwa mantiki hii serikali, Asasi za kiraia, na jamii ni
lazima kuhakikisha kuwa zinaweka mazingira rafiki (mazuri) kwa maendeleo yao na
kushiriki kikamilifu katika Nyanja za kisiasa, kiuchumi, kijamii na
kiutamaduni”. Alisema Mkurugenzi wa Asasi
ya Maendeleo ya vijana (TYPs-ASSOCIATION) Bwn. Japheth M. Kurwa
“Ili vijana
waweze kunufaika na fursa za maendeleo ikiwemo mikopo itolewayo na serikali ni
lazima wakizi vigezo stahili ambavyo ni pamoja na: usajiri angalau kwa ngazi ya
Halmashauri, wawe na miradi na iwe halisi, miradi hiyo iwe rafiki wa mazingira,
iwe na uwezo wa kupunguza umasiki, uelewa wa kikundi juu ya miradi hiyo,
uwezekano wa mradi kulipa mkopo ndani ya miaka miwili, uwiano wa mkopo na mradi
wenyewe, na upatikanaji wa soko la mazao ya miradi yao. Mikopo hii inalenga
maendeleo ya vijana kwenye miradi hivyo ni muhimu kutambua kuna wajibu wa
kufanya ili kunufaika na mikopo hiyo”. Alisema
Ngudu Adolfu Kami, Afisa maendeleo ya vijana-Manispaa ya Musoma
“Kwa vijana
wasio katika vikundi yya maendeleo, watengeneze vikundi ili kukizi vigezo vya
kunufaika na fursa zinazokuja moja kwa moja kwenye vikundi na sio kwa mmoja
mmoja. Na vikundi vyote vya maendeleo ya vijana viwe na njozi ya kujitengenezea
fursa za ajira ili kupunguza umasikini uliokithiri. Vikundi ni lazima vijenge
tabia ya uzalishaji na uwekezaji ili kuzalisha mitaji kwani vijana wengi ni
wazuri kwa uzalishaji na matumizi hii haitawasaidia. Pia ni wakati sasa vikundi
wa kuwa wanachama kwenye SACCOS ya Vijana na SACCOS nyingine ili viweze kupata
mikopo ya mitaji kwa riba nafuu”. Alisema
Ngugu Masatu Rugee, Afsa michezo na
utamaduni Halimashauri ya wilaya ya Musoma.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !