TANZANIA YOUTH POTENTIALS ASSOCIATION
(TPYs-ASSOCIATION), Asasi ya maendeleo ya vijana yenye makao yake katika
manispaa ya Musoma imewakutanisha vijana wapatao 87 na Shilika la Swiss Contact
lenye makao makuu yake inchini Swaziland chini ya mradi wake wa U-Learn Program
unaowalenga vijana wenye umri kati ya miaka 15-25. Malengo ya mradi huo ni
vijana kuweza kujiajiri, hivyo hutoa elimu na mafunzo ya ufundi kwa vijana.
“Naamini maendeleo ya vijana yataletwa na vijana
wenyewe, wakishikwa mkono na wadau wa maendeleo yao, akiwemo mdau mkuu ambaye ni serikali, lakini vijana
hatuna budi kuijua Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana na kusimamia
utekelezaji wake kwenye Nyanja mbalimbali kuanzia kwenye maeneo tunayoishi hadi
serikali kuu. Kwa hali ya kutokuwa na
ufadhiri tunafanya kazi kwa kujituma, nidhamu, kujitoa kwa wito; na
kujitahidi kuwakutanisha vijana na fursa mbalimbali za maendeleo yao wakiwemo
wadau mbalimbali wa maendeleo ya vijana”. Alisema Bwana Japheth M.
Kurwa-Mkurugenziwa Asasi
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !