TWAWEZA KUONDOA UKATILI WA AINA ZOTE DHIDI YA WANAWAKE
Monday, August 19, 2013
ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI YATOLEWA KWA VIJANA WA MIAKA 15-25 MANISPAA YA MUSOMA
Sunday, August 18, 2013
TANZANIA YOUTH POTENTIALS ASSOCIATION
(TPYs-ASSOCIATION), Asasi ya maendeleo ya vijana yenye makao yake katika
manispaa ya Musoma imewakutanisha vijana wapatao 87 na Shilika la Swiss Contact
lenye makao makuu yake inchini Swaziland chini ya mradi wake wa U-Learn Program
unaowalenga vijana wenye umri kati ya miaka 15-25. Malengo ya mradi huo ni
vijana kuweza kujiajiri, hivyo hutoa elimu na mafunzo ya ufundi kwa vijana.
“Naamini maendeleo ya vijana yataletwa na vijana
wenyewe, wakishikwa mkono na wadau wa maendeleo yao, akiwemo mdau mkuu ambaye ni serikali, lakini vijana
hatuna budi kuijua Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana na kusimamia
utekelezaji wake kwenye Nyanja mbalimbali kuanzia kwenye maeneo tunayoishi hadi
serikali kuu. Kwa hali ya kutokuwa na
ufadhiri tunafanya kazi kwa kujituma, nidhamu, kujitoa kwa wito; na
kujitahidi kuwakutanisha vijana na fursa mbalimbali za maendeleo yao wakiwemo
wadau mbalimbali wa maendeleo ya vijana”. Alisema Bwana Japheth M.
Kurwa-Mkurugenziwa Asasi
VIKUNDI VYA SANAA YA UIGIZAJI KUJENGEWA UWEZO-MUSOMA
Pichani-kulia (picha ya
mkono wa kushoto mwenye) t-shirt ni M/Kiti wa kikundi cha Nyota Sanaa Group
ndugu Majura Majura akicheza mchezo wa kuigiza na timu ya MINIBUZZ-Toa hoja!. Kwenye soko la Nyakato-Musoma. Katika ziara yao
mjini Musoma. Kikundi hiki ni baadhi ya vikundi vya maendeleo ya vijana
vinavyijishughulisha na sanaa ya uigizaji walivyovitembelea na kuigiza nao kwa
kuwajengea uwezo. TYPS-ASSOCIATION (ASASI YA MAENDELEO YA VIJANA) inajumla ya
vukundi 31 vya maendeleo ya vijana
TYPs-ASSOCIATION KUENDESHA MAFUNZO YA UJASILIAMALI
Pichani ni kikundi cha
maendeleo ya vijana kilichopo kijiji cha Ryamisanga, Kata ya Bwiregi, Wilayani
Butiama-Mara. Aliyesimama, mwenye t-shirt ya njano ni Mwl. Magta Nyangore
(Mwezeshaji wa elimu ya ujasiliamali kwa program ya “Kazi Nje Nje” ya ILO). Mafunzo hayo yalitolewa kwa ushirikiano na
Asasi ya TYPs-ASSOCIATION kwa mkakati wake wa kutekeleza Sera ya Taifa ya
Maendeleo ya Vijana.
WiLDAF KUONGEZA UWEZO KWA MAKUNDI YA WANAWAKE NA ASASI ZA KUTETEA HAKI ZA WANAWAKE-MUSOMA
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgg_6rBgP0ix8qpqMhzF84jpwmMokMQVU31KIx5YXckTy0nmsFvfM8wbTfmU8KSuBbuvnak4kgLrXsjiWaZaiot7zCCFGUT9Z2FySiQ5nabVJcMGnHb52BNZcTqX01GThcYwzZbLgSh-Jm0/s320/WiLDAF+Workshop.jpg)
Warsha hiyo
iliendeshwa na na Asasi ya Women in Law and Development in Africa (WiLDAF). WiLDAF ni mtandao, na Tanzania makao makuu yake yako
Dar es Salaam, Mikocheni. Kila raia ana wajibu wa kufanya ili kulinda haki zake
vinginevyo haki zake huweza kuvunjwa. Alisema mwezeshaji Destalia Haule kutoka
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC). Bwana Aliko Sengo mwezeshaji toka
WiLDAF aliseme elimu hii washiriki waliyoipata waipeleke katika jamii, na kutoa
kisha wito
VIJANA KUKUTANA NA FURSA ZA MAENDELEO-MUSOMA
Pichani
ni viongozi wa vikundi vya maendeleo ya vijana (vikundi 31) kutoka wilaya za
Butiama na Musoma wakiwa na maafisa wa serikali na Asasi za kiraia katika picha
ya pamoja ndani ya viwanja vya Kituo cha Matumaini katika Vijana-Manispaa ya
Musoma
Maafisa hao ni
pamoja na: Ndugu Adolfu Kami wa kwanza kushoto waliosimama mstari wa kwanza,
afisa maendeleo ya vijana manispaa ya Musoma, ndugu Masatu Rugee, afisa michezo
na utamaduni halimashauli ya wilaya ya Musoma, Afisa utawala na Fedha Ndugu
Robert Moro, wa Shirika la Kutetea Haki za Wanawake na Watoto (ABC FOUNDATION);
na Ndugu George Muyabi mratibu wa Mara Development Forum (MDF), pamoja na afisa
mmoja wa CHODAWU na Idara ya Kazi na Ajira-Musoma
Asasi
iliwakutanisha viongozi wa vikundi vya maendeleo ya vijana (vikundi 31) na
maafisa hao kwa lengo la vijana hao kutambua fursa na wajibu wao ili waweze
kunufaika na fursa zilizo katika ofsi za idara hizo za serikali
“Kila kijana ni
muhimu kutambua haki na wajibu wake; kila kijana ana haki na wajibu wa
kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo yake bifsi, ya jamii pamoja
na taifa kwa ujumla. Na kwa mantiki hii serikali, Asasi za kiraia, na jamii ni
lazima kuhakikisha kuwa zinaweka mazingira rafiki (mazuri) kwa maendeleo yao na
kushiriki kikamilifu katika Nyanja za kisiasa, kiuchumi, kijamii na
kiutamaduni”. Alisema Mkurugenzi wa Asasi
ya Maendeleo ya vijana (TYPs-ASSOCIATION) Bwn. Japheth M. Kurwa
“Ili vijana
waweze kunufaika na fursa za maendeleo ikiwemo mikopo itolewayo na serikali ni
lazima wakizi vigezo stahili ambavyo ni pamoja na: usajiri angalau kwa ngazi ya
Halmashauri, wawe na miradi na iwe halisi, miradi hiyo iwe rafiki wa mazingira,
iwe na uwezo wa kupunguza umasiki, uelewa wa kikundi juu ya miradi hiyo,
uwezekano wa mradi kulipa mkopo ndani ya miaka miwili, uwiano wa mkopo na mradi
wenyewe, na upatikanaji wa soko la mazao ya miradi yao. Mikopo hii inalenga
maendeleo ya vijana kwenye miradi hivyo ni muhimu kutambua kuna wajibu wa
kufanya ili kunufaika na mikopo hiyo”. Alisema
Ngudu Adolfu Kami, Afisa maendeleo ya vijana-Manispaa ya Musoma
“Kwa vijana
wasio katika vikundi yya maendeleo, watengeneze vikundi ili kukizi vigezo vya
kunufaika na fursa zinazokuja moja kwa moja kwenye vikundi na sio kwa mmoja
mmoja. Na vikundi vyote vya maendeleo ya vijana viwe na njozi ya kujitengenezea
fursa za ajira ili kupunguza umasikini uliokithiri. Vikundi ni lazima vijenge
tabia ya uzalishaji na uwekezaji ili kuzalisha mitaji kwani vijana wengi ni
wazuri kwa uzalishaji na matumizi hii haitawasaidia. Pia ni wakati sasa vikundi
wa kuwa wanachama kwenye SACCOS ya Vijana na SACCOS nyingine ili viweze kupata
mikopo ya mitaji kwa riba nafuu”. Alisema
Ngugu Masatu Rugee, Afsa michezo na
utamaduni Halimashauri ya wilaya ya Musoma.
Blog Archive
-
▼
2013
(21)
-
▼
August
(7)
- TWAWEZA KUONDOA UKATILI WA AINA ZOTE DHIDI YA WANA...
- ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI YATOLEWA KWA VIJANA WA ...
- VIKUNDI VYA SANAA YA UIGIZAJI KUJENGEWA UWEZO-MUSOMA
- TYPs-ASSOCIATION KUENDESHA MAFUNZO YA UJASILIAMALI
- WiLDAF KUONGEZA UWEZO KWA MAKUNDI YA WANAWAKE NA A...
- VIJANA KUKUTANA NA FURSA ZA MAENDELEO-MUSOMA
- “WATANZANIA TUJITATHMINI NA SIASA ZETU”
-
▼
August
(7)
Followers
Blog Archive
-
▼
2013
(21)
-
▼
August
(7)
- TWAWEZA KUONDOA UKATILI WA AINA ZOTE DHIDI YA WANA...
- ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI YATOLEWA KWA VIJANA WA ...
- VIKUNDI VYA SANAA YA UIGIZAJI KUJENGEWA UWEZO-MUSOMA
- TYPs-ASSOCIATION KUENDESHA MAFUNZO YA UJASILIAMALI
- WiLDAF KUONGEZA UWEZO KWA MAKUNDI YA WANAWAKE NA A...
- VIJANA KUKUTANA NA FURSA ZA MAENDELEO-MUSOMA
- “WATANZANIA TUJITATHMINI NA SIASA ZETU”
-
▼
August
(7)