Karibu Musoma Information Center kwa huduma zifuatazo:- 1) Kwa kutengenezewa design mbalimbali kama za Business card, Vipeperushi, mabango mbalimbali, kadi za Harusi za kisasa zaidi, kadi za mialiko mbalimbali, Vitambulisho vya wanafunzi wa sekondari na katika kampuni mbalimbali ( ID cards) na kadi nyinginezo zenye design ya kuvutia. 2) Kutengenezewa mabango ( Posters) mbalimbali zinazohusu biashara ya mhusika au bidhaa mbalimbali. 3) Kutengenezewa nembo ( LOGO) za kuhusiana kampuni au biashara yako. 4) Tunatengeneza tovuti ( Websites ) zenye kiwango ambacho huwezi amini kama zinatengenezwa musoma, kwa bei nafuu ambayo huwezi ipata kwingine isipo kuwa kwetu. 5) Mwisho tunatoa ushauri na elimu kuhusiana na maswala ya computer.5) Sisi ni watengenezaji wa blog zinazokaa mfumo wa website. kama hii unayoiona.

Welcome to TYPS - ASSOCIATION

Welcome to TYPS - ASSOCIATION

Welcome

A Letter from the Executive Director

Dear All,

As Executive Director it is my pressure to welcome you to TANZANIA YOUTH POTENTIALS ASSOCIATION (TYPs-ASSOCIATION)-a growing youth-led Organization with it’s headquarter in Musoma that operates through legal registration number 00NGO/00006304 under the ACT of 2002 in Tanzania. The focus of the organization is to utilize youth’s potentials for their own development, community and state development at large. It also intends to strengthen regional and international interventions towards protection and promotion of the human rights especially to children, youth and women. It works with networking with other partners/ stakeholders and beneficiaries.

The Organization has the mission of striving and inheriting youth and other community groups with various technical capacities eligible to make them be engines for socio-economic growth for individual benefits, societies and the national at large as such to see a community in which women’s and children’s rights are observed and respected by executing mobilization projects eligible to bring positive changes to community through action and participation in collaboration with community and other stakeholders to prevent Gender Based Violence (GBV).

However the organization is dedicated to develop dynamic and entrepreneurial youths who will engage and realize their full potential and that of their community, their country and the world at large and advocating The National Youth Development Policy

The Secretariat , the Board of Directors and the Annual General Meeting of TYPs-ASSOCIATION eagerly anticipate your arrival and contribution to its future, and welcome you to discover youth development experience that promotes your Personal and intellectual growth

Welcome to TYPs-ASSOCIATION,
Mr. Japheth M. Kurwa
Executive Director


UZINDUZI: SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA 2014

Friday, November 21, 2014



Umma wa watanzania wanaharakati wa kupinga vitendo vya Ukatili wa Kijinsia jumanne tarehe 25, Novemba 2014 watazindua kampeni hii kitaifa, kimkoa na maeneo mbalilmbali ya kiutendaji.  Hii ni kampeni ya siku 10 na huzinduliwa tarehe 25, Novemba ya kila mwaka hadi tarehe 10, Desemba.

Kitaifa itazinduliwa pale Viwanja vya Karimjee kuanzia saa 3 asubuhi. Uzinduzi huu utafuatana  na maandamano ya amani yakihamasisha jamii kuachana na Vitendo vya Ukatili wa Kijinsia, kuanzia viwanja vya mnazi mmoja kupitia, barabara ya Morogoro, barabara ya Bibi Titi Mohamed, Ali Hassan Mwinyi,Mtaa wa Ohio, Samora hadi Viwanja vya Karimjee. Yote haya yataanza saa 1:30 asubuhi.

Kauli Mbiu ya mwaka huu ni “FUNGUKA! FICHUA UKATILI WA KIJINSIA KWA AFYA YA JAMII” ,Katika Kiingereza, “OPEN UP! DISCLOSE GENDER BASED VIOLENCE FOR THE HEALTH OF THE COMMINITY”

Kampeni hii kitaifa inaratibiwa na Shirika na WiLDAF kwa kushirikiana na Wadau toka Irish AID na UN Women.

Watanzania tupinge Vitendo vyote vya Ukatili wa Kijinsia, vitendo hivi huongeza mzigo kwa maendeleo ya jinsi zote, familia, jamii husika na taifa kwa ujumla.

AJIRA: VIJANA AMBAO HAWAKUBAHATIKA KUENDELEA NA MASOMO.




Kundi hili ni kundi linalojumuisha vijana wengi zaidi kuliko lile la vijana wasomi. Vijana wengi walioko katika kundi hili ni wale walioko katika ajira zisizo lasmi kama vile; uvuvi, kilimo, kubeba mizigo, ufugaji, machinga, garage, udereva wa magari na pikipiki (Bodaboda), ulinzi, vibarua vya ujenzi, vibarua katika sekta ya madini, migahawa/ vibanda vya lishe na kuchoma chips, saloon, uselemala, vibarua viwandani n.k
1.   Tafsiri Baadhi ya Maneno
Ajira: Ni shughuli yoyote halali (rasmi au isiyo rasmi), inayomwezesha mwananchi kujipatia riziki, mahitaji na kipato cha kuendesha maisha yake, ya familia na pengine kuchangia katika pato la eneo alipo au Taifa.
Kutokuwa na ajira: Ni hali ya kukosa kazi kabisa au nguvukazi iliyopo kutotumika kuzalisha mali au kutoa huduma.
 Kijana: Zipo tafsiri aina mbili;
i)    Kimataifa; Kijana ni mtu mwenye umri wa miaka 15 hadi 24
ii)   Kwa Tanzania ni miaka 15 hadi 35
Sekta isiyo rasmi: Hii ni sekta ambayo si ya shambani wala ofisini, ya kiwango cha chini na ya kujiajiri   inayotumia mtaji na teknolojia ndogo.
Fursa: Ni shughuli za kiuchumi na kijamii au za uzalishaji mali au huduma ambazo hutekelezwa na mtu na kuweza kumpatia kipato halali.

2.   Fursa ya Uvuvi na Uzaji wa Samaki-Kisiwani Lukuba
Sekta ya Uvuvi ni moja ya sekta iliyoajiri vijana wengi hapa Tanzania, Kisiwa cha lukuba ni moja ya Visiwa vilivyoko mkoani Mara chenye fursa kubwa ya ajira ya kujiajiri.
Kisiwa hiki kinatoa fursa nyingi za ajira ya kujiajiri kwa vijana hususani wale ambao hawakubahatika kwendelea na masomo. Fursa za ajira ni uvuvi unaoambatana na usafirishaji, uchakataji, uchuuzi wa samaki na uzalishaji viwandani, ujenzi wa mitumbwi/boti za uvuvi.
Kisiwa hiki kinategemea shughuli ya uvuvi na uuzaji wa samaki hususani samaki aina ya Dagaa na Sangara (Nile perch). Uvuvi katika kisiwa hiki unatoa mchango mkubwa katika kuinua kiwango cha maisha ya vijana hawa, wananchi wa Musoma na nchi kwa ujumla. Hata hivyo, fursa bado ni kubwa kwa wawekezaji wengi kuwekeza katika eneo hili.
Serikali inatakiwa kuongeza juhudi za makusudi kuhakikisha uendelevu wa raslimali ya uvuvi ambayo ni msaada mkubwa kwa taifa. Aidha inatakiwa kuliangalia eneo hili kwa makini ili kuwawezesha vijana hususani kundi hili ambalo halikubahatika kuendelea na masomo yao.

3.   Changamoto ya Jumla Kuhusu Ajira ya Vijana ambao Hawakubahatika Kuendelea na Masomo.
Kundi hili ni kundi linalojumuisha vijana wengi zaidi kuliko lile la vijana wasomi, kwa mtazamo wa haraka kundi hili la vijana ni kama limesahulika.; changamoto zinazolikabili kundi hili ni pamoja na:-
·         Hali ya kutokuwa na fursa ya kushiriki katika uchumi inayosababishwa na uwezo mdogo katika mitaji, ukosefu wa ujuzi na uzoefu wa biashara, pamoja na matatizo yanayohusiana na kutokopesheka.
·         Hali ya kutopata fursa ya kushiriki katika fursa za kiuchumi katika mfumo rasmi
·         Kutopokelewa na jamii katika mtazamo chanya; kunakoleta tafasili kandamizi kwao kama vile tafasiri ya wahuni na watu waliofeli maisha, tafasili ambayo hupelekea vijana hao kuwa hivyo.
·         Uhusiano mdogo wa kundi hili na sekta rasmi, taasisi binafsi na za umma; na Serikali kwa ujumla

4.   Nini Kifanyike
Wadau wote wa maendeleo ya vijana (serikali, jamii, sekta binafsi, Asasi za kijamii, familia na vijana wenyewe) kuwa karibu sana na kundi hili kama walezi na walimu; na kutekeleza wajibu huu ipasavyo

Vijana kuchangamkia fursa na kuzitumia ipasavyo katika kuwekeza na kuzalisha (Saving and Production). Ogopeni semi kama vile: Tumia pesa ikuzoee, elfu moja haijengi, raha jipe mwenyewe, kula ujana maisha yenyewe mafupi n.k

Maeneo haya yenye kuwaajiri vijana walioko katika kundi hili, yakipewa kipaumbile na kutengenezwa kuwa mazingira rafiki ya kujiajiri yatapunguza kwa kiasi kikubwa kero ya ajira kwa vijana na taifa kwa ujumla.

By: Mr. Japheth M. Kurwa
Falsafa yangu ni:- “JUHUDI ZISIZOKOMA KATIKA KUJIFUNZA NA KUFANYA KAZI”

MAENDELEO YA VIJANA: TUNAO WAJIBU WA KUFANYA

Thursday, October 16, 2014

Utangulizi
  Changamoto ya maendeleo ya vijana ni suala mtambuka. Uwezeshaji wa vijana unajumuisha juhudi za pamoja za wadau mbalimbali muhimu pamoja na serikali, jamii, sekta binafsi, asasi za kijamii, familia na vijana wenyewe.
  Kwa mujibu wa sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007; vijana fasili yake ni Vijana wa kiume na kike kuanzia umri wa miaka 15 hadi 35.
Wadau wa Maendeleo ya Vijana
Wadau wa maendeleo ya vijana ni pamoja na:-
  • Serikali
  • Jamii
  • Sekta binafsi
  • Asasi za kijamii
  • Familia
  • Vijana wenyewe
Kada, Ofisi, Idara na Taasisi za Umma Zinazoshughulika moja kwa moja na Masuala/ Maendeleo ya Vijana
  Kada/ofisi ya Maendeleo ya Vijana; inaratibu masuala yote ya vijana
  Kada/ofisi ya Utamaduni
  Kada/ofisi ya Michezo
  Kada/ofisi ya Maendeleo ya Jamii; kwa usajiri wa Vikundi
  Kada/ofisi ya Ushirika; ushauri wa kitaalam na kisheria kuhusu ushirika wa vikundi kama vile SACCOS, VICOBA n.k na Usajili
  Idara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana
  VETA
Fursa za Vijana toka Serikalini
  Mfuko wa Taifa wa Maendeleo ya Vijana; unatoa mikopo kwa vikundi vya maendeleo ya vijana nchini kote kupitia SACCOS za Vijana zinazoendelea kuudwa na vijana wenyewe kila halmashauri nchini
  Mradi wa kufyatua Tofari wa Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) kwa halimashauri zote nchini
  Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF); unatoa mikopo ya mitaji kwenye SACCOS zikiwemo zile za Vijana
  Halmashauri; zina mfuko wa kukopesha/ kuwawezesha vikundi vya wanawake na vijana kupitia ofisi ya mtendaji wa kata na Kamati za Maendeleo ya Kata(WDC) n.k
Wosia kwa Vijana na Wadau wa Wamaendeleo ya Vijana
  Taifa halimuangalii kijana kama tatizo bali kama rasilimali na nguvukazi ya kujenga uchumi wa Taifa
  Taifa linatambua ushindani mkubwa wa kimaendeleo baina ya vijana na ubunifu walionao
  Kuna kila haja ya kuwekeza zaidi katika ubunifu wa vijana (Youth initiatives) ili waweze kujiajiri na kuajiri vijana wenzao.
  Tunao wajibu wakufanya; ikiwa ni pamoja na kuchangamkia fursa zote za maendeleo na kuzitumia vizuri.
  Kwa changamoto ya mitaji inayotukabili vijana; tukumbuke umoja ni nguvu  hivyo yatupasa kuunda/ kuanzisha ushirika ili kuweza kupata mitaji
  Vijana wengi hawana mahusiano mazuri na sekta rasmi, hivyo kila mdau atambue anao wajibu wa kufanya ili kusaidia suala la maendeleo ya vijana; hususani kijana mwenyewe

TUNAWEZA: MIRADI YA KILIMO

Monday, July 28, 2014





Kikundi cha TUNAWEZA ni ushirika wa hiari wa ujasiriamali wa kilimo, ufugaji na biashara kwa maendeleo ya wanakikundi, kikundi, jamii na taifa kwa ujumla. Kikundi hiki kipo Mtaa wa Kiara, Kata ya Kigera, Manispaa ya Musoma.

Katibu wa kikundi, Japheth M. Kurwa alisema yafuatayo “Tunaimani juu ya kilimo, na kwa sasa tunayo miradi miwili ya kilimo; wa kwanza ni mradi wa kilimo cha Mhogo katika eneo la Kisiwani-Kiara lililoko wilayani Manispaa ya Musoma, na kwa mradi huu tunazo ekari 5, na mradi wa pili ni kilimo cha zao la biashara la mahindi, katika eneo la bonde la mto Suguti lililoko wilayani Bunda mkoani Mara. Tunazo hekari 15 za mahindi tutakazolima msimu.

Miradi yote hii tunajikita katika kuzalisha katika hali ya ubora na ufanisi ili kupunguza balaa la njaa katika jamii na kwa taifa kwa ujumla, ikiwa ni pamoja na wanakikindi kujiajiri katika kilimo.

Pamoja na jitihada zote hizi katika kilimo bado tunakabiliwa na changamoto ya ukosefu mitaji ili tuweze kuwekeza na kuzalisha kwa ufanisi mkubwa. Tunaupungufu wa pembejeo za kilimo na nyenzo za kisasa ambayo huadhili miradi hii kwa kiasi kikubwa.

Changamoto ya pili ni ya mabadiliko ya tabia nchi, hii inatulazimu kununua machine za umwagiliaji kwani mvua sasa ni tatizo.
Kama kikundi tunayo mikakati madhubuti ya kuweza kupata mikopo na kwa sasa tumekwisha omba toka Halmashauri ya Manispaa ya Musoma kupitia fedha za vijana-Katani kufadhili mradi wa kilimo cha Muhogo, pia temeomba fedha toka Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo kupitia mfuko wa maendeleo ya vijana. Lakini pia wanakikundi tunao utaratibu wa kuchangia miradi hii. Mwenyezi Mungu akitujaharia kupata fedha hizi tunaamini kupitia kilimo tutafanya mambo makubwa.

Si sahihi kuwa na dhana kwamba kilimo cha biashara kinaweza kufanywa na watu wenye kipato cha kati na cha juu. Tumeanza mwaka jana miradi yote hii na sasa tumeona kuwa inawezekana na TUNAWEZA kwani wazo tunalo, watu tunao na kwa umoja wetu tutaujenga uchumi wetu”.

VIJANA MANISPAA YA MUSOMA KUAZIMIA KUUNDA CHAMA CHA AKIBA NA MIKOPO

Monday, April 14, 2014





CHAMA CHA USHIRIKA CHA AKIBA NA MIKOPO CHA VIJANA MUSOMA SACCOS (VIMU SACCOS) LTD
S.L.P …., Musoma-Mara. Simu: 0756290672, 0755671818, & 0654655498

Vijana wapatao 45, manispaa ya Musoma wameazimia kuunda na kusajiri Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo kijulikanacho kwa jina la VIJANA MUSOMA SACCOS LTD kwa lengo la kuinuana khali zao kiuchumi na kijamii.
Mwenyekiti wa Bodi ya uanzilishi wa Chama hicho, Bwn. Japheth M. Kurwa; alisema “Wanachama wa chama cha ushirika cha VIJANA MUSOMA SACCOS (VIMU SACCOS) tumeamua rasmi na kwa dhati kusaidiana, kushirikiana, kuthaminiana, kujaliana, kujiendeleza na kusimamia ubora wa maisha yetu ili kila mmoja apate unafuu na furaha katika maisha kwa kuzingatia misingi ya uhuru, haki, udugu na amani, Madhumuni ya chama hiki cha ushirika ni kuinua na kuimarisha hali ya kiuchumi na kijamii ya wanachama wake (Vijana) kwa kufuata kanuni na taratibu za vyama vya ushirika. Hivyo basi napenda kutoa wito kwa vijana wote wa manispaa ya Musoma kujiunga na Chama hiki. Vijana Musoma SACCOS ni kwa Ajiri ya Maendeleo yako Binafsi, Familia yako, Jamii yako, na Taifa kwa Ujumla.
“Weka Akiba Mara kwa Mara, Kopa kwa Busara, Lipa Upesi”

Followers

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. TZ Youth Potentials - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Inspired by Sportapolis Shape5.com
Proudly powered by Blogger