MIDAHALO YA WAZI NA SINEMA KUZUIA UKATILI WA KIJINSIA

Thursday, September 26, 2013

TYPs-ASSOCIATION (Asasi ya Maendeleo ya Vijana na Haki za Wanawake na Watoto) wakishirikiana na SHirika ya ABC Foundation(Shirika la Kutetea Haki za Wanawake na Watoto) chini ya kampeni ya TUNAWEZA. Kampeni hii iliweza Asasi na wadau mbalimbali kuvunja ukimya juu ya ukatili majumbani na jamii kuona kwamba ukatili si sehemu ya maisha, hata hivyo jamii ilitambua maana, aina na nini kifanyike kutokomeza ukatili wa kijinsia/nyumbani.
Kampeni ya TUNAWEZA Tanzania inasimamiwa na Oxfam, WLAC, KIVULINI na Haki Madini ikitekelezwa na wadau mbalimbali wa mashirika haya, ikiwa ni pamoja na ABC Foundation (Shirika la Kutetea Haki za Wanawake na Watoto) chini ya Shirika la KIVULINI. Lengo Kuu la Kampeni ya Tunaweza: Kupunguza Ile Khali ya Jamii Kuona Ukatili ni Kitendo cha Kawaida au ni Sehemu ya Maisha. Jamii itambue kuwa kwa pamoja tunaweza kuondoa aina zote za ukatili wa kijinsia/nyumbani.
 
Sambamba na midahalo hiyo jioni iliambatana na maenesho ya sinema za kupinga ukatili wa kijinsia/nyumbani kama vile Neria na Narando.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Followers

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. TZ Youth Potentials - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Inspired by Sportapolis Shape5.com
Proudly powered by Blogger