Wanachama wa
chama cha ushirika cha VIJANA MUSOMA
SACCOS (VIMUSA) tumeamua rasmi na kwa dhati kusaidiana, kushirikiana,
kuthaminiana, kujaliana, kujiendeleza na kusimamia ubora wa maisha yetu ili
kila mmoja apate unafuu na furaha katika maisha kwa kuzingatia misingi ya
uhuru, haki, undugu na amani.
ENEO LA SHUGHULI
Eneo la
shughuli za chama ni wilaya ya Musoma mjini, lakini hata wanachama walioko nje ya eneo la wilaya
watashiriki kama wataweza kushiriki kikamilifu katika shughuli za chama
MADHUMUNI
Madhumuni ya
chama hiki cha ushirika ni kuinua na kuimarisha hali ya kiuchumi na kijamii ya
wanachama wake kwa kufuata kanuni na taratibu za vyama vya ushirika. Ili
kufanikisha madhumuni haya, ushirika huu
wa Akiba na Mikopo utafanya yafuatayo:-
a)
Kuhamasisha wanachama wake kujenga tabia ya kujiwekea akiba
mara kwa mara
b)
Kupokea na kutunza akiba na amana za wanachama kwa njia
rahisi na salama
c)
Kutafuta vyanzo vya fedha ili kujenga na kuimarisha
mtaji kwa ajili ya kutoa mikopo kwa
wanachama kwa masharti na riba nafuu
d)
Kuwaelimisha wanachama kujijengea tabia ya kukopa kwa busara
na kutumia vizuri mikopo na kuinua hali zao za maisha kiuchumi na kijamiii.
e)
Kutoa bidhaa mbalimbali za fedha(financial products) kwa
wanachama ili waweze kushiriki zaidi kuimarisha mitaji ya chama na mitaji yao
binafsi ili waweze kuleta mvuto kwa wasio wanachama kujiunga na chama
f)
Kuweka kwa usalama fedha za chama na za wanachama kwa
kuanzisha mipango kwa kukabiliana na
majangana/au kuweka bima za fedha zinazofaa
g)
Kuwashauri wanachama
kuandaa mipango yao ya maendeleo katika kuwekeza mitaji kwenye miradi ya
kiuchumi na huduma za jamii
h)
Kutoa elimu ya ushirika kwa wanachama
i)
Kufanya mambo mengine ambayo yataendeleza hali ya uchumi wa
chama na wanachama
j)
Kuwaelimisha wanachama umuhimu wa kutumia fedha zao kwa
mipango, kuweka hakiba, kukopa kwa ajiri maendeleo ya biashara na kilimo kupiga
vita tabia ya ufujaji mali na matumizi mabaya ya fedha
UANACHAMA
Mtu yeyote
anaweza kuwa mwanachama akiwa na sifa zifuatazo:-
a)
Awe na umri usiopungua miaka 18. Mtu yeyote mwenye umri
usiopungua miaka 15 anaweza kuwa mwanachama isipokuwa hataruhusiwa kukgombea
uongozi na kukopa mpaka atakapotimiza miaka 18
b)
Awe na akili timamu
na tabia njema
c)
Awe anafanya kazi au shughuli yoyote halali na awe mkazi wa
eneo la chama na kufuata masharti ya chama
d)
Awe tayari kushiriki kikamilifu katika shughuli zote za
chama
e)
Asiwe na shughuli binafsi zinazofanana na shughuli za chama
f)
Kikundi/Chama/Taasisi/Asasi yenye sifa za kujiunga na chama
hiki kwa mujibu wa sheria ya vyama vya ushirika,kanuni za vyama vya ushirika
pamoja na masharti haya
g)
Awe mfanyakazi au mtumishi wa chama
h)
Awe amelipa kiiingilio
(5,000/-)na kununua kima cha chini cha hisa
(Hisa 1@ 10,000/-)
CHANGAMOTO
Kuna
changamoto kubwa kwa vijana kama wanufaika:-
Ø
Vijana wengi
hawapo katika ngazi za maamuzi, matokeo yake maamuzi mengi hayagusi matakwa ya
vijana
Ø
Vijana wengi
hawana utayari ulio thabiti na wa kweli, wa kushiriki kuibua fursa na kuzitumia
ipasavyo
Ø
Vijana wengi hasa
miji midogo hawana tabia ya “kuwekeza na kuzalisha”, wengi wanadesturi ya
kutumia kidogo walichonacho kwa kauli kama vile: tumia pesa ikuzoee, elfu moja
haijengi n.k
Bado
hatujachoka,ni kwamba vijana hawana elimu ya ujamaa(umoja na udugu) na
kujitegemea tutazidi kuwahamasisha vijana kutumia fursa ya SACCOS ya vijana manispaa ya Musoma kwa maana
ya VIJANA MUSOMA SACCOS (VIMUSA) kujiunga
na SACCOS hii yenye nia ya kukuza mitaji kwa vijana ili waweze kujiajiri.
“Weka
Akiba Mara kwa Mara, Kopa kwa Busara, Lipa Upesi”
Japheth
M. Kurwa
Mob: 0756290672 & 0712547199 Email: kurwajapheth@gmail.com
Mwenyekiti, VIMUSA
Mob: 0756290672 & 0712547199 Email: kurwajapheth@gmail.com
Mwenyekiti, VIMUSA
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !