Kijana Esogo Kubega, mkazi wa
Kigera-Manispaa ya Musoma, akijibidisha katika shughuli za kilimo cha bustani
kama ajira yake. Japo mafanikio yapo lakini nina changamoto kubwa ya maji kwani
maji haya ni ya dibwini na upatikana kwa muda mfupi tu mara baada ya musimu wa
mvua, Mungu akinifungulia milango nikapata kuchimba kisima cha kudumu na
mashine ya kumwagilia naamini sitokuwa na haja ya kuajiliwa kwani hapa ndipo
penye riziki yangu. Lakini pia nina changamoto ya magonjwa, mwaka jana nililima
tikiti maji zikashambuliwa na wadudu na mwaka huuu nimebadilisha na kulima
nyanya nako tazama zilivyoshambuliwa na wadudu, hii yote ni ukosefu wa mitaji.
Mbona mkoa wa Mara sera ya kilimo kwanza siioni au ni maalumu kwa mikoa Fulani
tu, kama ni ya kitaifa basi itukumbuke nasi pia twahiitaji, Alisema Kijana
Esogo Kubega.
Napenda kumshukuru Bw. Kurwa,
mkurugenzi wa Asasi ya Maendeleo ya Vijana na Haki za Wanawake na Watoto (TYPs-ASSOCIATION) kwa kutuwezesha kupata elimu
ya ujasilia mali kwa kiasi kikubwa elimu hii imetupa mwanga mkubwa wa kazi zetu
za kilimo na ujasilia mali. Wakipatikana watu kama hawa 10 mbona ukombozi kwa
vijana umepatikana. Ugumu ni kujitafutia mtaji mwenyewe na khali huna hata mia
mfukoni kwangu mimi mtaji ni kikwazo kikubwa sana ningekuwa mbali, Esogo
alizidi kusema. Picha na TYPs-ASSOCIATION
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !