Kutunza AMANI ni jukumu la kila Mtanzania

Friday, June 14, 2013

Ni jukumu la kila mtanzania kulinda amani tuliyopewa kama zawadi na mwenyezi Mungu ili kumwenzi Baba wa Taifa letu ambaye ndiye aliyesimama kidete na kutoka na nguvu alizo pewa na mwenyezi mungu ili kuweza kukomboa watu wake kutoka katika utumwa ambao ulikuwa umewagubika watanzania. Hivyo basi kila mmoja wetu asimame imara katika kuitetea, kuiheshimu na kuilinda amani yetu ambayo ndio nembo yatu kwa mataifa mbalimbali .
Tanzania ni nchi ya pekee inayosifika kwa amani duniani na hii ni kutokana na nguvu kubwa iliyofanywa na baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere. Na kweli kwa enzi zake kulikuwa hakuna haja ya kujiuliza maswali juu ya amani yetu. Lakini kwanzia tumpoteze Mwasisi wetu amani yetu imekuwa ikiyumba yumba kila kukicha kwa sababu kumekuwa kukitokea matatizo na matukio ya uharifu kila kikicha na hiki ni kiashirio tosha cha kushuka kwa amani yetu.
 Nawaasa watanzania wote waone kama kutunza amani ni jukumu la kila mtanzania na si Serikali pekee.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Followers

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. TZ Youth Potentials - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Inspired by Sportapolis Shape5.com
Proudly powered by Blogger