KIKOSI cha Taifa Stars kitashuka dimbani keshokutwa Jumapili kuivaa
Ivory Coast katika mechi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2014, lakini
habari ni kuwa kiungo mshambuliaji wa Stars, Mrisho Ngassa hataruhusiwa
kucheza kwa kuwa ana kadi mbili za njano.
Taarifa ambazo Championi
Ijumaa imezipata kutoka ndani ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),
zimesema kuwa wamepokea ujumbe kutoka Shirikisho la Soka Afrika (Caf)
kuwa Ngassa ana kadi mbili za njano.
Taarifa hiyo imesema kuwa,
kiungo huyo alipata kadi mbili za njano katika michezo miwili ya
nyumbani na ugenini wakati Stars ikiumana na Morocco, ambapo mchezo wa
kwanza uliopigwa Machi, Stars ilishinda mabao 3-1 kabla ya kupokea
kichapo cha mabao 2-1 ugenini.
“Tumepokea ujumbe kutoka Caf juu ya
Ngassa, ni taarifa mbaya hasa katika siku hizi mbili kwa sababu tunajua
kocha alikuwa anajua atakuwa naye katika mchezo wa keshokutwa,” alisema
kiongozi huyo wa TFF.
Aidha, straika wa Stars, Mbwana Samatta: “Ile
ni timu tu (Ivory Coast) kama timu nyingine, sijaona sababu za kuiogopa
au kuihofia, tuna asilimia kibao za kushinda ukizingatia tunacheza
nyumbani, ” alisema Samatta.
HomeNGASSA kuikosa Ivory Coast.
NGASSA kuikosa Ivory Coast.
Friday, June 14, 2013
You might also like this post
Blog Archive
-
▼
2013
(21)
-
▼
June
(7)
- CLOUDS FM YAKANUSHA KUHUSU MWANA FA KUAHIRISHA SHO...
- NGASSA kuikosa Ivory Coast.
- Baba mzazi wa Langa aweka wazi chanzo cha kifo ch...
- Kutunza AMANI ni jukumu la kila Mtanzania
- AFRICAN BARRICK GOLD WATOA MILION 10 KWA REDS MISS...
- Huyu ndiye mtoto wa miaka 14 wa kitanzania anayete...
- Polisi Afukuzwa Kazi kwa Kupiga picha za Uchi Mago...
-
▼
June
(7)
Followers
Blog Archive
-
▼
2013
(21)
-
▼
June
(7)
- CLOUDS FM YAKANUSHA KUHUSU MWANA FA KUAHIRISHA SHO...
- NGASSA kuikosa Ivory Coast.
- Baba mzazi wa Langa aweka wazi chanzo cha kifo ch...
- Kutunza AMANI ni jukumu la kila Mtanzania
- AFRICAN BARRICK GOLD WATOA MILION 10 KWA REDS MISS...
- Huyu ndiye mtoto wa miaka 14 wa kitanzania anayete...
- Polisi Afukuzwa Kazi kwa Kupiga picha za Uchi Mago...
-
▼
June
(7)
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !