MIDAHALO YA WAZI NA SINEMA KUZUIA UKATILI WA KIJINSIA
Thursday, September 26, 2013
TYPs-ASSOCIATION (Asasi ya Maendeleo ya Vijana na Haki za Wanawake na Watoto) wakishirikiana na SHirika ya ABC
Foundation(Shirika la Kutetea Haki za Wanawake na Watoto) chini ya kampeni ya TUNAWEZA. Kampeni hii iliweza Asasi na wadau mbalimbali kuvunja ukimya juu ya ukatili majumbani na jamii kuona kwamba ukatili si sehemu ya maisha, hata hivyo jamii ilitambua maana, aina na nini kifanyike kutokomeza ukatili wa kijinsia/nyumbani.
Kampeni ya TUNAWEZA Tanzania
inasimamiwa na Oxfam, WLAC, KIVULINI na Haki Madini ikitekelezwa na wadau
mbalimbali wa mashirika haya, ikiwa ni pamoja na ABC Foundation (Shirika la
Kutetea Haki za Wanawake na Watoto) chini ya Shirika la KIVULINI. Lengo Kuu la
Kampeni ya Tunaweza: Kupunguza Ile Khali ya
Jamii Kuona Ukatili ni Kitendo cha Kawaida au ni Sehemu ya Maisha. Jamii
itambue kuwa kwa pamoja tunaweza kuondoa aina zote za ukatili wa
kijinsia/nyumbani.
KILIMO KAMA MKOMBOZI WA VIJANA NI CHANGAMOTO
Thursday, September 19, 2013
Napenda kumshukuru Bw. Kurwa,
mkurugenzi wa Asasi ya Maendeleo ya Vijana na Haki za Wanawake na Watoto (TYPs-ASSOCIATION) kwa kutuwezesha kupata elimu
ya ujasilia mali kwa kiasi kikubwa elimu hii imetupa mwanga mkubwa wa kazi zetu
za kilimo na ujasilia mali. Wakipatikana watu kama hawa 10 mbona ukombozi kwa
vijana umepatikana. Ugumu ni kujitafutia mtaji mwenyewe na khali huna hata mia
mfukoni kwangu mimi mtaji ni kikwazo kikubwa sana ningekuwa mbali, Esogo
alizidi kusema. Picha na TYPs-ASSOCIATION