Karibu Musoma Information Center kwa huduma zifuatazo:- 1) Kwa kutengenezewa design mbalimbali kama za Business card, Vipeperushi, mabango mbalimbali, kadi za Harusi za kisasa zaidi, kadi za mialiko mbalimbali, Vitambulisho vya wanafunzi wa sekondari na katika kampuni mbalimbali ( ID cards) na kadi nyinginezo zenye design ya kuvutia. 2) Kutengenezewa mabango ( Posters) mbalimbali zinazohusu biashara ya mhusika au bidhaa mbalimbali. 3) Kutengenezewa nembo ( LOGO) za kuhusiana kampuni au biashara yako. 4) Tunatengeneza tovuti ( Websites ) zenye kiwango ambacho huwezi amini kama zinatengenezwa musoma, kwa bei nafuu ambayo huwezi ipata kwingine isipo kuwa kwetu. 5) Mwisho tunatoa ushauri na elimu kuhusiana na maswala ya computer.5) Sisi ni watengenezaji wa blog zinazokaa mfumo wa website. kama hii unayoiona.

Welcome to TYPS - ASSOCIATION

Welcome to TYPS - ASSOCIATION

Welcome

A Letter from the Executive Director

Dear All,

As Executive Director it is my pressure to welcome you to TANZANIA YOUTH POTENTIALS ASSOCIATION (TYPs-ASSOCIATION)-a growing youth-led Organization with it’s headquarter in Musoma that operates through legal registration number 00NGO/00006304 under the ACT of 2002 in Tanzania. The focus of the organization is to utilize youth’s potentials for their own development, community and state development at large. It also intends to strengthen regional and international interventions towards protection and promotion of the human rights especially to children, youth and women. It works with networking with other partners/ stakeholders and beneficiaries.

The Organization has the mission of striving and inheriting youth and other community groups with various technical capacities eligible to make them be engines for socio-economic growth for individual benefits, societies and the national at large as such to see a community in which women’s and children’s rights are observed and respected by executing mobilization projects eligible to bring positive changes to community through action and participation in collaboration with community and other stakeholders to prevent Gender Based Violence (GBV).

However the organization is dedicated to develop dynamic and entrepreneurial youths who will engage and realize their full potential and that of their community, their country and the world at large and advocating The National Youth Development Policy

The Secretariat , the Board of Directors and the Annual General Meeting of TYPs-ASSOCIATION eagerly anticipate your arrival and contribution to its future, and welcome you to discover youth development experience that promotes your Personal and intellectual growth

Welcome to TYPs-ASSOCIATION,
Mr. Japheth M. Kurwa
Executive Director


CLOUDS FM YAKANUSHA KUHUSU MWANA FA KUAHIRISHA SHOW YAKE YA THE FINEST LEO HII

Friday, June 14, 2013

Clouds FM yakanusha KUHUSU  MWANA FA  KUAHIRISHA SHOW YAKE  YA THE FINEST  LEO HII.Baada ya  mtandao Feki wa facebook utumiao jina lake kuandika kuwa show hiyo  imeahirishwa.
Chanzo cha habari Udakuespecially

NGASSA kuikosa Ivory Coast.

KIKOSI cha Taifa Stars kitashuka dimbani keshokutwa Jumapili kuivaa Ivory Coast katika mechi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2014, lakini habari ni kuwa kiungo mshambuliaji wa Stars, Mrisho Ngassa hataruhusiwa kucheza kwa kuwa ana kadi mbili za njano.
Taarifa ambazo Championi Ijumaa imezipata kutoka ndani ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), zimesema kuwa wamepokea ujumbe kutoka Shirikisho la Soka Afrika (Caf) kuwa Ngassa ana kadi mbili za njano.
Taarifa hiyo imesema kuwa, kiungo huyo alipata kadi mbili za njano katika michezo miwili ya nyumbani na ugenini wakati Stars ikiumana na Morocco, ambapo mchezo wa kwanza uliopigwa Machi, Stars ilishinda mabao 3-1 kabla ya kupokea kichapo cha mabao 2-1 ugenini.
“Tumepokea ujumbe kutoka Caf juu ya Ngassa, ni taarifa mbaya hasa katika siku hizi mbili kwa sababu tunajua kocha alikuwa anajua atakuwa naye katika mchezo wa keshokutwa,” alisema kiongozi huyo wa TFF.
Aidha, straika wa Stars, Mbwana Samatta: “Ile ni timu tu (Ivory Coast) kama timu nyingine, sijaona sababu za kuiogopa au kuihofia, tuna asilimia kibao za kushinda ukizingatia tunacheza nyumbani, ” alisema Samatta.

Baba mzazi wa Langa aweka wazi chanzo cha kifo cha mwanae


Baba mzazi we Langa, Mangisemi Kileo ameeleza chanzo cha kifo cha mwanaye ambaye kimetokea jana katika Hospitali ya Muhimbili.Langa amefariki dunia jana katika hospitali ya Muhimbili baada ya kulazwa usiku wa kuamkia jana.
Imeelezwa Langa alifikishwa hospitalini hapo akiwa amezidiwa na moja kwa moja akafikishwa katika chumba cha watu mahututi.
Salehjembe ilifika nyumbani kwao marehemu eneo la Mikocheni Regency dakika chache baada ya taarifa za msiba na kuzungumza na baba yake mzazi, Mengiseni Kileo.
Kileo alisema Langa alizidiwa ghafla juzi, wakamkibiza katika Hospitali ya Kairuki.
“Pale walituambia kwamba anasumbuliwa maralia kali pamoja na ugonjwa wa uti wa mgongo.

“Hivyo tukalazimika kumkimbiza Muhimbili ambako alifikishwa katika chumba cha watu matuhuti (ICU), leo ndiyo mauti yamemkuta,” alisema.

Kuhusiana na mazishi, Kileo alisema wanalazimika kumsubiri mkewe, Venus ambaye anatarajia kutua nchini kesho au keshokutwa.

“Mama yake yuko Marekani, hivyo tutamsubiri lakini tumeshazungumza naye.

“Sisi tutakaa leo kujadili suala hilo na wanafamilia na baadaye tutajua kila kitu,” alisema Kileo akionyesha utulivu.




Langa alikuwa akitamba na nyimbo yake mpya ya Rafiki wa Kweli iliyotengenezwa katika studio za Bongo Record chini ya P Funk.
Msanii huyo alianza kutamba baada ya kushinda usakaji vipaji chini ya Coca Cola na kuunda kundi la Wakilisha akiwa na Shaa au Sarah na Witness wakianza na wimbo wao wa kwanza ‘Hoi’.

Kutunza AMANI ni jukumu la kila Mtanzania

Ni jukumu la kila mtanzania kulinda amani tuliyopewa kama zawadi na mwenyezi Mungu ili kumwenzi Baba wa Taifa letu ambaye ndiye aliyesimama kidete na kutoka na nguvu alizo pewa na mwenyezi mungu ili kuweza kukomboa watu wake kutoka katika utumwa ambao ulikuwa umewagubika watanzania. Hivyo basi kila mmoja wetu asimame imara katika kuitetea, kuiheshimu na kuilinda amani yetu ambayo ndio nembo yatu kwa mataifa mbalimbali .
Tanzania ni nchi ya pekee inayosifika kwa amani duniani na hii ni kutokana na nguvu kubwa iliyofanywa na baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere. Na kweli kwa enzi zake kulikuwa hakuna haja ya kujiuliza maswali juu ya amani yetu. Lakini kwanzia tumpoteze Mwasisi wetu amani yetu imekuwa ikiyumba yumba kila kukicha kwa sababu kumekuwa kukitokea matatizo na matukio ya uharifu kila kikicha na hiki ni kiashirio tosha cha kushuka kwa amani yetu.
 Nawaasa watanzania wote waone kama kutunza amani ni jukumu la kila mtanzania na si Serikali pekee.

AFRICAN BARRICK GOLD WATOA MILION 10 KWA REDS MISS MARA

Ofisa kutoka kitengo cha Mawasiliano na
Mahusiano wa Barrick Gold Mining Fatuma Mssumi akimkabidhi Kaimu Ofisa Tawala
wa Mkoa wa Mara mfano wa hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 10, ikiwa ni
sehemu ya udhamini wa kampuni hiyo kwenye mashindano la Redd’s Miss Mara
yatakayofanyika leo mjini Musoma.
Baadhi ya washiriki wa shindano la Redd’s Miss
Mara 2013 wakiwa katika picha ya pamoja jana ikiwa ni siku moja kabla ya
warembo hao hawajapanda jukwaani kuwania taji hilo ambalo linashikiliwa na Miss
Tanzania namba mbili 2012. Shindano hilo linataraji kufanyika leo.

 Baadhi ya washiriki wa Redd’s Miss Mara 2013 wakiwa wenye furaha.
Baadhi ya warembo wakiwa katika pozi
Baadhi ya washiriki wa shindano la Redd’s Miss
Mara 2013 wakitembea kwa pamoja leo ikiwa ni siku moja kabla ya
warembo hao hawajapanda jukwaani kuwania taji hilo ambalo linashikiliwa na Miss Tanzania namba mbili 2012. Shindano hilo linataraji kufanyika leo.

Huyu ndiye mtoto wa miaka 14 wa kitanzania anayetengeneza application za simu na kuwauzia nokia

Tuesday, June 11, 2013

 

Alvin Walter Makundi ni kijana mdogo wa Kitanzania anayeishi na wazazi wake nchini Singapore. Akiwa na umri wa miaka 14 na mwanafunzi wa kidato cha pili huko Singapore, tayari ameshatumbukiza jina lake katika orodha ya wataalamu wa application katika moja ya makampuni makubwa duniani ya kutengeneza simu za mkononi ya NOKIA, ambapo anatengeneza applications ambazo anazituma katika kampuni hiyo ambayo nayo bila hiana huitumia.

Polisi Afukuzwa Kazi kwa Kupiga picha za Uchi Magomeni

POLISI wa kike wa Kituo cha Magomeni, jijini Dar es Salaam aliyejulikana kwa jina moja la Anisa, ametimuliwa kazi  kwa madai ya kupiga picha ya utupu iliyosambaa mitandaoni.
Chanzo makini ndani ya jeshi hilo kilisema Anisa alifukuzwa kazi wiki iliyopita baada ya kuhojiwa na mabosi wake wa makao makuu ya jeshi hilo na kukiri kuwa picha hiyo ni yake.
“Anisa aliitwa makao makuu, mabosi wakamuonesha picha yake akiwa mtupu kitandani, akakiri ni yeye. Alijitetea eti alifanya hivyo kwa sababu siku ya tukio alikuwa amelewa sana,” kilisema chanzo.
Chanzo kiliendelea kudai kwamba baada ya afande huyo mwenyeji wa Tanga kukiri, viongozi wa jeshi hilo walimwambia amekiuka kanuni na kulidhalilisha jeshi hilo hivyo hataendelea kuwa mtumishi.
Picha ya afande huyo imeenea mitandaoni na kwenye baadhi ya simu za mikononi za watu kitendo kulicholifanya jeshi hilo kufanya uchunguzi na kubaini kuwa ni yake.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina, Suleiman Kova alipoulizwa  juzi alikiri kufukuzwa kwa askari huyo na kumtaka mwandishi wetu kufuatilia zaidi kwa Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Camilius Wambura ambaye naye alipoulizwa kuhusu tukio hilo alikiri.
‘‘Tunahitaji askari wenye maadili mema ndani ya jeshi letu, yule atakayefanya mambo bila kufuata kanuni na sheria hatua kali zitachukuliwa dhidi yake. Askari muda wote anatakiwa awe mfano bora kwa  jamii,’’ alisema Afande Wambura.
Taarifa zaidi zinadai kwamba kwa sasa Anisa anaishi uraiani kama raia wa kawaida.

Followers

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. TZ Youth Potentials - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Inspired by Sportapolis Shape5.com
Proudly powered by Blogger