PROGRAM YA UHAMASSHAJI NA MAFUNZO KWA VIJANA.

Friday, January 9, 2015



PROGRAM YA UHAMASSHAJI NA MAFUNZO KWA VIJANA.
Katika mikakati ya kuhamasisha vijana na kuwawezesha kiuchumi, na kijamii, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imeandaa na kuendesha program ya mafunzo kwa vijana.  Tar 22-24, Desemba 2014 maafisa wa wizara walikuwa mkoani Arusha wakitoa mafunzo hayo kwa halimashauri ya Arusha Jiji, Arusha DC, Meru na Monduli.
Kutokana na umuhimu wa mafunzo haya halimashauri zilizobaki zinatakiwa kuendesha mafunzo haya ifikapo Februari 30, 2015, kwa kushirikiana na maafisa wa mkoa na halmashauri husika. Mada zilizofundishwa ni pamoja na:-
             i.        Sera ya taifa ya maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007
            ii.        Stadi za maisha
           iii.        Dhima ya uanzishwaji wa SACCOS za vijana
           iv.        Mwongozo wa uandaaji katiba
            v.        Mwongozo wa utoaji wa mikopo ya mfuko wa maendeleo ya vijana kwenye miradi
           vi.        Usajiri wa vikundi vya vijana
         vii.        Namna ya kuandika miradi
Mada zote nimeziambatanishwa jiandaeni kufanikisha zoezi hili. Aidha mambo ya msingi yatokanayo ni:-
     i.        Mikopo ya vijana toka mfuko wa vijana unaosimamiwa na wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Kwa kuanzia wizara imetenga kiasi cha shilingi milioni 30 kwa vikundi 3 kila halmashauri na fedha hizo zitapita kwenye SACCOS za vijana.
    ii.        Uanzishwaji wa SACCOS ya vijana kwa kila halimashauri. Mpaka sasa ni halimashauri tatu tu zilizotekeleza agizo hili kati ya halmashauri saba; ambazo ni halmashauri ya Karatu; SIMBA MASAI SACCOS LTD, Halmashauri ya Meru; MERU VIJANA SACCOS LTD; na Halmashauri ya Longido; LONGIDO VIJANA SACCOS LTD.
Halmashauri zilizokwisha sajiri SACCOS za vijana ifikapo tarehe 30 Januari, 2015 ziwe zimekwisha wasilisha maandiko ya miradi yasiopungua manne kwa Afisa Maendeleo ya Vijana Mkoa tayari kutumwa wizarani.
Sambamba na haya utekelezaji wa agizo la Rais katika sherehe za maadhimisho ya kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru 2014 mkoani Tabora kuhusu maswala ya vijana ikiwa ni pamoja na zoezi la uanzishwaji wa SACCOS za Vijana kama ifuatavyo:-
             i.        Kutenga 5% ya mapato ya halmashauri kwa ajili ya kuwawezesha vijana. Naomba utekelezaji wake ipasavyo.
            ii.        Maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli za vijana ili kujikwamua kiuchumi; hususani shughuli za kilimo na biashara.

"VIJANA TUNAO WAJIBU WA KUFANYA"
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Followers

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. TZ Youth Potentials - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Inspired by Sportapolis Shape5.com
Proudly powered by Blogger