Katika mikakati ya kuhamasisha vijana na kuwawezesha kiuchumi, na kijamii, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imeandaa na kuendesha program ya mafunzo kwa vijana. Tar 22-24, Desemba 2014 maafisa wa wizara walikuwa mkoani Arusha wakitoa mafunzo hayo kwa halimashauri ya Arusha Jiji, Arusha DC, Meru na Monduli.
PROGRAM YA UHAMASSHAJI NA MAFUNZO KWA VIJANA.
Friday, January 9, 2015

Kutokana na umuhimu wa mafunzo haya halimashauri zilizobaki
zinatakiwa kuendesha mafunzo haya ifikapo Februari 30, 2015, kwa kushirikiana na maafisa wa mkoa na halmashauri husika. Mada
zilizofundishwa ni pamoja na:-
i.
Sera ya taifa ya maendeleo ya Vijana ya
mwaka 2007
ii.
Stadi za maisha
iii.
Dhima ya uanzishwaji wa SACCOS za vijana
iv.
Mwongozo wa uandaaji katiba
v.
Mwongozo wa utoaji wa
mikopo ya mfuko wa maendeleo ya vijana kwenye miradi
vi.
Usajiri wa vikundi vya vijana
vii.
Namna ya kuandika miradi
Mada zote nimeziambatanishwa jiandaeni
kufanikisha zoezi hili. Aidha mambo ya msingi yatokanayo ni:-
i.
Mikopo ya vijana toka mfuko wa vijana
unaosimamiwa na wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Kwa kuanzia wizara
imetenga kiasi cha shilingi milioni 30 kwa vikundi 3 kila halmashauri na fedha
hizo zitapita kwenye SACCOS za vijana.
ii.
Uanzishwaji wa SACCOS ya vijana kwa kila
halimashauri. Mpaka sasa ni halimashauri tatu tu zilizotekeleza agizo hili kati
ya halmashauri saba; ambazo ni halmashauri
ya Karatu; SIMBA MASAI SACCOS LTD, Halmashauri ya Meru; MERU VIJANA SACCOS LTD;
na Halmashauri ya Longido; LONGIDO VIJANA SACCOS LTD.
Halmashauri
zilizokwisha sajiri SACCOS za vijana ifikapo tarehe 30 Januari, 2015 ziwe zimekwisha wasilisha maandiko ya miradi yasiopungua manne kwa Afisa Maendeleo
ya Vijana Mkoa tayari kutumwa wizarani.
Sambamba
na haya utekelezaji wa agizo la Rais katika sherehe za maadhimisho ya kilele
cha mbio za Mwenge wa Uhuru 2014 mkoani Tabora kuhusu maswala ya vijana ikiwa
ni pamoja na zoezi la uanzishwaji wa SACCOS za Vijana kama ifuatavyo:-
i.
Kutenga 5% ya mapato ya halmashauri kwa
ajili ya kuwawezesha vijana. Naomba utekelezaji wake ipasavyo.
ii.
Maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli za
vijana ili kujikwamua kiuchumi; hususani shughuli za kilimo na biashara.