TANLAP YATOA MAFUNZO YA WATU WENYE ULEMAVU NA USULUHISHI MBADALA WA MIGOGORO
Saturday, March 29, 2014
Mtandao wa watoa msaada wa
kisheria (TANZANIA NETWORK OF LEGAL AID PROVIDERS-TANLAP) inaendesha mafunzo ya
sheria ya watu wenye ulemavu na usuluhishi mbadala wa migogoro, kwa wanachama
wake wapatao 60. Mafunzo yamefanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 27/3/2014
hadi 29/3/2014 katika Hotel ya Tamal jijini Dar es Salaam.
ü Siku
ya Kwanza: 27/3/2014: Sheria ya Watu wenye Ulemavu
ü Siku
ya Pili: 28/3/2014: Utatuzi wa Migogoro Kutumia Njia Mbadala
ü Siku
ya Tatu: 29/3/2014: Utatuzi Mbadala ya
Migogoro
Bwn. Gideoni Mandesi (Wakili),
kama mwezeshaji wa mafunzo sheria ya watu wenye ulemavu akifafanua Sheria Na. 9
ya mwaka 2010 alieleza makundi 7( Upofu, viungo, akili, kiziwi, ulemavu wa
ngozi, , uono hafifu na ulemavu wa viungo) ya walemavu na kusisitiza kwamba
pamoja na uwepo wa sheria hii Asasi za kiraia zina wajibu kisheria wa kufanya
ili sheria hii iwasaidie walengwa, na kusisitiza misingi ya sheria hii (Kifungu cha 4. (a)-(g) kama ifuatavyo.
a) Kuheshimu
utu, uhuru wa mtu
b) Kutobaguliwa
c) Kushurikishwa
katika nyaja zote katika jamii
d) Usawa
wa fursa
e) Ufikikaji
f) Usawa
wa kijinsia kwa kutambua haki na mahitaji ya walemavu
g) Kutoa
usalama na ulinzi wa kijamii
Adhabu kwa Unyanyapaa wa Walemavu
1) Kwa taasisi; faini isiyo chini ya shilingi
millioni mbili(2,000,000/=) na
isiyopungua shilingi million ishirini (20,000,000/=)
2) Kwa mtu binafsi; faini isiyopungua shilingi
laki tano (500,000/=) na isiyozidi shilingi milioni saba(7,000,000/=) au
Kufungwa jela
mwaka mmoja au vyote kwa pamoja
Bwn James Marenga (wakili),
mwezeshaji wa usuluhishi mbadala wa migogoro. Alitoa hatua 7 za ukuaji wa
migogoro
1) Kutokuwepo
taarifa na takwimu sahihi
2) Mahusiano
3) Thamani
4) Muundo
5) maslahi
Aidha alisisitiza ni vizuri na muhimu sana kila sahuli lipitie hatua ya usuluhishi mbadala wa migogoro kabla ya shauri hilo kwenda kwenye ngazi za mahakama na sheria inalitambua hilo na kulipa uzito. na kuwataka washiriki hao ambao ni wanachama wa mtandao huo kutumia njia mbadala wa usuluhishi wa migogoro kabla ya mashauri hayo kwenda mahakamani akibainisha na faida zake katika tathnia ya sheria.