Siku 16 za harakati dhidi ya
ukatili wa kijinsia ni kampeni ya kimataifa iliyoanzishwa na taasisi ya
kimataifa ya wanawake katika uongozi “ Womens Global Leadership Institute” ,
iliyoanzishwa mwaka 1991 nchini Marekani kwa nia ya kuamsha Ari ya kuzuiana
kupambana na ukatili dhidi ya wanawake, kwa kuzingatia haya ya kuleta usawa wa
kijinsia.
Kampeni hii ilianzishwa ikiwa ni
matokeo ya mauaji ya wanawake yaliyotokea 1960 Mirabele inchini Dominica,
wanawake hawa wakiwa katika harakati za kupinga utawala wa kidikteta wa Rais
wan chi hiyo Ndugu Raphaeli Truijilo, na kuhitimishwa tarehe 10 Desemba ambayo
ni siku ya kimataifa la tamko la haki za binadamu, ikiwa ni ishara ya kuhusisha
ukatili dhidi ya wanawake na haki za binadamu, kwani ukatili huu ni uvunjivu wa
haki za binadamu
Kati ya tarehe 25/11/ hadi Tarehe
10/12 ya kila mwaka, kuna matukio mbalimbali ya kimataifa, ambayo ni sehemu
muhimu katika kuleta ukombozi kwa jamii, hasa wanawake juu ya ukatili wa
kijinsia. Baada ya matukio hayo, ni pamoja na siku ya kimataifa ya wanawake
watetezi wa haki za binadamu 29/11 ya kila mwaka, Desemba 1 siku ya UKIMWI
duniani, Desemba 6 kumbukumbu ya mauaji ya kikatili ya wanawake wahandisi mjini
Montreal nchini Canada, tarehe 30 Desemba siku ya kidunia ya Kampeni ya
Tunaweza, inayolenga kuondoa ukatili wa aina zote dhidi ya wanawake na Desemba
10 siku ya tamko la haki za binadamu kimataifa
Kwa sababu hizi siku 16 za
harakati za kupinga unyanyasaji wa kijinsia duniani huazimishwa Novemba 25-
Desemba 10 kila mwaka.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !