Karibu Musoma Information Center kwa huduma zifuatazo:- 1) Kwa kutengenezewa design mbalimbali kama za Business card, Vipeperushi, mabango mbalimbali, kadi za Harusi za kisasa zaidi, kadi za mialiko mbalimbali, Vitambulisho vya wanafunzi wa sekondari na katika kampuni mbalimbali ( ID cards) na kadi nyinginezo zenye design ya kuvutia. 2) Kutengenezewa mabango ( Posters) mbalimbali zinazohusu biashara ya mhusika au bidhaa mbalimbali. 3) Kutengenezewa nembo ( LOGO) za kuhusiana kampuni au biashara yako. 4) Tunatengeneza tovuti ( Websites ) zenye kiwango ambacho huwezi amini kama zinatengenezwa musoma, kwa bei nafuu ambayo huwezi ipata kwingine isipo kuwa kwetu. 5) Mwisho tunatoa ushauri na elimu kuhusiana na maswala ya computer.5) Sisi ni watengenezaji wa blog zinazokaa mfumo wa website. kama hii unayoiona.

Welcome to TYPS - ASSOCIATION

Welcome to TYPS - ASSOCIATION

Welcome

A Letter from the Executive Director

Dear All,

As Executive Director it is my pressure to welcome you to TANZANIA YOUTH POTENTIALS ASSOCIATION (TYPs-ASSOCIATION)-a growing youth-led Organization with it’s headquarter in Musoma that operates through legal registration number 00NGO/00006304 under the ACT of 2002 in Tanzania. The focus of the organization is to utilize youth’s potentials for their own development, community and state development at large. It also intends to strengthen regional and international interventions towards protection and promotion of the human rights especially to children, youth and women. It works with networking with other partners/ stakeholders and beneficiaries.

The Organization has the mission of striving and inheriting youth and other community groups with various technical capacities eligible to make them be engines for socio-economic growth for individual benefits, societies and the national at large as such to see a community in which women’s and children’s rights are observed and respected by executing mobilization projects eligible to bring positive changes to community through action and participation in collaboration with community and other stakeholders to prevent Gender Based Violence (GBV).

However the organization is dedicated to develop dynamic and entrepreneurial youths who will engage and realize their full potential and that of their community, their country and the world at large and advocating The National Youth Development Policy

The Secretariat , the Board of Directors and the Annual General Meeting of TYPs-ASSOCIATION eagerly anticipate your arrival and contribution to its future, and welcome you to discover youth development experience that promotes your Personal and intellectual growth

Welcome to TYPs-ASSOCIATION,
Mr. Japheth M. Kurwa
Executive Director


VIJANA MUSOMA SACCOS (VIMUSA)

Tuesday, November 19, 2013


Wanachama wa chama cha ushirika cha VIJANA MUSOMA SACCOS (VIMUSA) tumeamua rasmi na kwa dhati kusaidiana, kushirikiana, kuthaminiana, kujaliana, kujiendeleza na kusimamia ubora wa maisha yetu ili kila mmoja apate unafuu na furaha katika maisha kwa kuzingatia misingi ya uhuru, haki, undugu na amani.

ENEO LA SHUGHULI
Eneo la shughuli za chama ni wilaya ya Musoma mjini, lakini  hata wanachama walioko nje ya eneo la wilaya watashiriki kama wataweza kushiriki kikamilifu katika shughuli za chama

MADHUMUNI
Madhumuni ya chama hiki cha ushirika ni kuinua na kuimarisha hali ya kiuchumi na kijamii ya wanachama wake kwa kufuata kanuni na taratibu za vyama vya ushirika. Ili kufanikisha madhumuni haya, ushirika  huu wa Akiba na Mikopo utafanya yafuatayo:-
a)      Kuhamasisha wanachama wake kujenga tabia ya kujiwekea akiba mara kwa mara
b)      Kupokea na kutunza akiba na amana za wanachama kwa njia rahisi na salama
c)      Kutafuta vyanzo vya fedha ili kujenga na kuimarisha mtaji  kwa ajili ya kutoa mikopo kwa wanachama kwa masharti na riba nafuu
d)      Kuwaelimisha wanachama kujijengea tabia ya kukopa kwa busara na kutumia vizuri mikopo na kuinua hali zao za maisha kiuchumi na kijamiii.
e)      Kutoa bidhaa mbalimbali za fedha(financial products) kwa wanachama ili waweze kushiriki zaidi kuimarisha mitaji ya chama na mitaji yao binafsi ili waweze kuleta mvuto kwa wasio wanachama kujiunga na chama
f)       Kuweka kwa usalama fedha za chama na za wanachama kwa kuanzisha  mipango kwa kukabiliana na majangana/au kuweka bima za fedha zinazofaa
g)       Kuwashauri wanachama kuandaa mipango yao ya maendeleo katika kuwekeza mitaji kwenye miradi ya kiuchumi na huduma za jamii
h)      Kutoa elimu ya ushirika kwa wanachama
i)        Kufanya mambo mengine ambayo yataendeleza hali ya uchumi wa chama na wanachama
j)        Kuwaelimisha wanachama umuhimu wa kutumia fedha zao kwa mipango, kuweka hakiba, kukopa kwa ajiri maendeleo ya biashara na kilimo kupiga vita tabia ya ufujaji mali na matumizi mabaya ya fedha

UANACHAMA
Mtu yeyote anaweza kuwa mwanachama akiwa na sifa zifuatazo:-
a)      Awe na umri usiopungua miaka 18. Mtu yeyote mwenye umri usiopungua miaka 15 anaweza kuwa mwanachama isipokuwa hataruhusiwa kukgombea uongozi na kukopa mpaka atakapotimiza miaka 18
b)       Awe na akili timamu na tabia njema
c)      Awe anafanya kazi au shughuli yoyote halali na awe mkazi wa eneo la chama na kufuata masharti ya chama
d)      Awe tayari kushiriki kikamilifu katika shughuli zote za chama
e)      Asiwe na shughuli binafsi zinazofanana na shughuli za chama
f)       Kikundi/Chama/Taasisi/Asasi yenye sifa za kujiunga na chama hiki kwa mujibu wa sheria ya vyama vya ushirika,kanuni za vyama vya ushirika pamoja na masharti haya
g)      Awe mfanyakazi au mtumishi wa chama
h)      Awe amelipa kiiingilio (5,000/-)na kununua kima cha chini cha hisa (Hisa 1@ 10,000/-)

CHANGAMOTO
Kuna changamoto kubwa kwa vijana kama wanufaika:-
Ø  Vijana wengi hawapo katika ngazi za maamuzi, matokeo yake maamuzi mengi hayagusi matakwa ya vijana
Ø  Vijana wengi hawana utayari ulio thabiti na wa kweli, wa kushiriki kuibua fursa na kuzitumia ipasavyo
Ø  Vijana wengi hasa miji midogo hawana tabia ya “kuwekeza na kuzalisha”, wengi wanadesturi ya kutumia kidogo walichonacho kwa kauli kama vile: tumia pesa ikuzoee, elfu moja haijengi n.k
Bado hatujachoka,ni kwamba vijana hawana elimu ya ujamaa(umoja na udugu) na kujitegemea tutazidi kuwahamasisha vijana kutumia fursa ya  SACCOS ya vijana manispaa ya Musoma kwa maana ya VIJANA MUSOMA SACCOS (VIMUSA) kujiunga na SACCOS hii yenye nia ya kukuza mitaji kwa vijana ili waweze kujiajiri.

“Weka Akiba Mara kwa Mara, Kopa kwa Busara, Lipa Upesi”

Japheth M. Kurwa
Mob: 0756290672 & 0712547199 Email: kurwajapheth@gmail.com
Mwenyekiti, VIMUSA

Followers

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. TZ Youth Potentials - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Inspired by Sportapolis Shape5.com
Proudly powered by Blogger