Karibu Musoma Information Center kwa huduma zifuatazo:- 1) Kwa kutengenezewa design mbalimbali kama za Business card, Vipeperushi, mabango mbalimbali, kadi za Harusi za kisasa zaidi, kadi za mialiko mbalimbali, Vitambulisho vya wanafunzi wa sekondari na katika kampuni mbalimbali ( ID cards) na kadi nyinginezo zenye design ya kuvutia. 2) Kutengenezewa mabango ( Posters) mbalimbali zinazohusu biashara ya mhusika au bidhaa mbalimbali. 3) Kutengenezewa nembo ( LOGO) za kuhusiana kampuni au biashara yako. 4) Tunatengeneza tovuti ( Websites ) zenye kiwango ambacho huwezi amini kama zinatengenezwa musoma, kwa bei nafuu ambayo huwezi ipata kwingine isipo kuwa kwetu. 5) Mwisho tunatoa ushauri na elimu kuhusiana na maswala ya computer.5) Sisi ni watengenezaji wa blog zinazokaa mfumo wa website. kama hii unayoiona.

Welcome to TYPS - ASSOCIATION

Welcome to TYPS - ASSOCIATION

Welcome

A Letter from the Executive Director

Dear All,

As Executive Director it is my pressure to welcome you to TANZANIA YOUTH POTENTIALS ASSOCIATION (TYPs-ASSOCIATION)-a growing youth-led Organization with it’s headquarter in Musoma that operates through legal registration number 00NGO/00006304 under the ACT of 2002 in Tanzania. The focus of the organization is to utilize youth’s potentials for their own development, community and state development at large. It also intends to strengthen regional and international interventions towards protection and promotion of the human rights especially to children, youth and women. It works with networking with other partners/ stakeholders and beneficiaries.

The Organization has the mission of striving and inheriting youth and other community groups with various technical capacities eligible to make them be engines for socio-economic growth for individual benefits, societies and the national at large as such to see a community in which women’s and children’s rights are observed and respected by executing mobilization projects eligible to bring positive changes to community through action and participation in collaboration with community and other stakeholders to prevent Gender Based Violence (GBV).

However the organization is dedicated to develop dynamic and entrepreneurial youths who will engage and realize their full potential and that of their community, their country and the world at large and advocating The National Youth Development Policy

The Secretariat , the Board of Directors and the Annual General Meeting of TYPs-ASSOCIATION eagerly anticipate your arrival and contribution to its future, and welcome you to discover youth development experience that promotes your Personal and intellectual growth

Welcome to TYPs-ASSOCIATION,
Mr. Japheth M. Kurwa
Executive Director


SERA YA TAIFA YA MAENDELEO YA VIJANA

Wednesday, July 24, 2013


SERA YA TAIFA YA MAENDELEO YA VIJANA
Sera hii iliandaliwa kwa ajili ya kusimamia maslahi ya kijana, ambayo serikali iliandaa mwaka 1996 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2007
Sera ya taifa ya maendeleo ya vijana ya 2007 inalenga masuala ya maendeleo ya vijana ambayo ni pamoja na: uwezeshaji wa kiuchumi, mazingira, VVU na Ukimwi, jinsia, sanaa na utamaduni, michezo afya ya uzazi kwa vijana na masuala ya maisha ya familia.
LENGO LA SERA
  • Kuhakikisha taifa linakuwa na vijana wenye uwezo, wenye ari ya kutosha , wawajibikaji na wanaoshiriki kikamilifu katika Nyanja zote za kijamii, kisiasa na kiuchumi kwa maendeleo ya jamii.
  • Kuweka mazingira yanayowezesha kujenga uwezo wa vijana na kukuza nafasi za ajira na kupata huduma ya hifadhi ya jamii
Kwa kifupi lengo ni kuwajengea uwezo, kuwawezesha na kuwaongoza vijana na wadau wenginekatika utekelezaji wa masuala ya maendeleo ya vijana
Sera ya taifa ya vijana imeandaliwa ili sisi vijana wa kike na wa kiumetuendelee kuleta msukumo wawa kuleta mageuzi ya kijamii, kiuchumi na kisiasa katika eneo lenye mabadiliko ya haraka duniani.
Maendeleo yetu ya kijamii yanategemea, pamoja na vitu vingine, ni kwa jinsi gani vijana tunahusika katika kujenga maisha ya baadaye. Hivyo ni kwa sababu hii sera inatuandaa kuwa viongozi, watoa uamuzi, wajasiriamali, wazazi na walezi kwa sababu tuna nafasi muhimu katika maendeleo ya jamii na uchumi wa taifa letu.
Sera ya taifa ya vijana imetoa maelekezo kwa vijana, washirikiane na wadau wengine katika masuala ya maendeleo yetu. Ila sera ni muongozo tu, utekelezaji wake ndio utakao tuwezesha kuvuna matunda ya sera hii nzuri .hatuna budi kuijua na kusimamia utekelezaji wake kwenye Nyanja mbalimbali kuanzia kwenye maeneo tunayoishi hadi serikali kuu
Wadau wote tushirikiane katika kutekeleza sere hii, hakika tutatengeneza vijana watakaolipeleka taifa hili mbele kimaendeleo (fema, APRIL-JUNE 2013.ONE DAY YES!, Youth POWER!, Zungumza na Mwanafunzi. Uk wa 2)

Simanzi familia za askari JWTZ

Thursday, July 18, 2013

 
Songea. Vilio na simanzi vimetawala katika baadhi ya familia za askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambao waliuwawa katika eneo la Darfur, Sudan ambako wanashiriki katika ulinzi wa amani.
Mamia ya waombolezaji walionekana katika makazi ya familia za marehemu; Songea mkoani Ruvuma na Nachigwea mkoani Lindi ambako ziko kambi ambazo baadhi ya askari hao walikuwa wakifanya kazi.
Imefahamika kuwa wanajeshi waliouwawa Jumamosi iliyopita wanatoka katika vikosi vya, 42KJ Chabruma, Songea,  44KJ Mbeya, 36KJ Msangani, 92KJ Ngerengere, 94KJ cha Mwenge, Dar es Salaam, 41KJ Nachingwea na Makao Makuu ya JWTZ- Upanga, Dar es Salaam.
Jana gazeti hili lilibaini kuwapo kwa maombolezo katika baadhi ya familia za wanajeshi hao baada ya kupokea taarifa za vifo vyao kutoka JWTZ. Hata hivyo bado majina ya waliofariki hayajawekwa hadharani.
Msemaji Mkuu wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe juzi aligoma kutaja majina hayo akisema kuwa majina hayo hayajatolewa rasmi na kwamba familia za marehemu zilikuwa hazijajulishwa.
“Hayo majina yanayotajwa kwenye mitandao ni ya uongo. Kwa sasa mimi sijaletewa majina na utaratibu uliopo ni hadi ‘next of kin’ (ndugu) wao wajulishwe kwanza,” alisema Kanali Mgawe.
Hata hivyo kupitia katika maeneo ilikokuwa misiba hiyo jana, gazeti hili lilifanikiwa kufahamu majina ya baadhi yao, ambayo yanafanana na yale yaliyotangazwa kwenye mitandao ya kijamii pamoja na baadhi ya magazeti.
Katika Kambi ya Chabruma, Songea mkoani Ruvuma kulikuwa na umati wa waombolezaji nyumbani kwa mmoja wa wapiganaji hao, Koplo Oswald Chaula ambaye alikuwa katika Kikosi cha Mizinga Chabruma na ndugu zake walikiri kupokea taarifa za msiba huo.
Hali kama hiyo ilikuwa nyumbani kwa Koplo Mohamed Chukilizo katika Kambi ya Majimaji, Nachingwea ambako baadhi ya ndugu na jamaa za zake wakiwamo mkewe na baba mkwe wake walikutana jana jioni kujadiliana kuhusu msiba.
Mwananchi pia lilishuhudia waombolezaji wakiwa wamekusanyika eneo la Mjimwema, Songea Mkoani Ruvuma ambako ni nyumbani kwa Komandoo Rodney Ndunguru aliyetoka kikosi cha 92KJ Ngerengere, Morogoro, baada ya kupokea taarifa za msiba huo. 
Vilio, Simanzi
Katika kambi ya Chabruma, mke wa marehemu Koplo Oswald aliyejitambulisha kwa jina la Maria alikuwa akilia kwa simanzi baada ya kupata taarifa kuwa miongoni mwa waliofariki ni baba watoto wake.

Followers

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. TZ Youth Potentials - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Inspired by Sportapolis Shape5.com
Proudly powered by Blogger